HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 10, 2022

Rais Dkt. Mwinyi afungua mkutano wa jukwaa la wahiri na kubainisha maeneo matano umuhimu kuhusu uchumi wa buluu



* TEF yaipongeza NSSF kwa kutoa msamaha wa tozo kwa waajiri wa sekta binafsi

Na MWANDISHI WETU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) huku akibainisha maeneo matano muhimu kuhusu uchumi wa buluu ambao ndio sera na muelekeo wa Serikali anayoiongoza.

Akifungua mkutano huo katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil mjini Zanzibar, Dkt. Mwinyi alisema uchumi wa buluu una sekta tano kubwa ikiwemo utalii, uvuvi na ufugaji wa samaki, bandari, usafiri na biashara za baharini pamoja na mafuta na gesi.

Rais Dkt. Mwinyi alisema hayo ndio maeneo muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi wa buluu ambapo alitumia fursa hiyo kulipongeza jukwaa la wahariri kwa uamuzi wake wa kuamua kufanya mkutano huo visiwani Zanzibar wenye kauli mbiu isemayo "Uchumi wa Buluu na Mawasiliano ya Umma.

Awali, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alizishukuru taasisi za Serikali ikiwemo NSSF kwa kuwaunga mkono katika mkutano huo.

Balile alisema NSSF inafanya mambo mengi mazuri hasa katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za wadau pamoja na kutatua changamoto za wanachama ambapo Bodi ya Wadhamini ya Mfuko ilitoa msamaha wa tozo kwa waajiri waliokuwa na malimbikizo ya michango kwa muda wa miezi mitatu na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 39 katika kipindi hicho.

Naye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alisema uamuzi wa jukwaa la wahariri kufanya mkutano wake Zanzibar ni ushahidi tosha kuwa Rais Dkt. Mwinyi anafanya kazi nzuri na kwamba wamekuja kuunga mkono mawazo ya Serikali yake ya kuifanya Zanzibar kuwa njema kupitia uchumi wa buluu.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari wa Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita alisema iko haja kwa wahariri kujifunza zaidi ili wanapotoa taarifa ziendane na zile sera za Serikali hasa kueleza maendeleo ya uchumi wa buluu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil mjini Unguja. Mara baada ya kuhutubia Mhe. Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alifungua rasmi mkutano huo. Mkutano huo umedhamiwa na taasisi mbalimbali ikiwemo NSSF ambayo ilipata fursa ya kutoa semina kwa wahariri kuhusu hifadhi ya jamii, majukumu na Utendaji wa Mfuko
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kupitia mkutano huo NSSF ni mdhamini mkuu.
Meneja Usimamizi Mafao  kutoka NSSF James Oigo akitoa mada kuhusu shughuli zinazofanywa na Mfuko wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambapo NSSF ndio mdhamini mkuu wa mkutano huo
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Iddrisa Kitwana Mustafa akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa  mwaka wa jukwaa la wahariri Tanzania uliofanyika Zanzibar 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape  Nnauye akizungumza na wahariri wakati  wa  Mkutano Mkuu wa  mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania uliofanyika Zanzibar 
Mwenyekiti  wa Jukwaa la  Wahariri Tanzania mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akiongea na wahariri na kushukuru Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuwa mdhamini  Mkuu wa mkutano wa mwaka  wa jukwaa  la wahariri Tanzania  uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na  Michezo Mhe. Tabia  Maulid Mwita, akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Balozi Ali Iddi Siwa cheti cha shukrani kwa Mfuko huo kudhamini Mkutano Mkuu wa TEF.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na viongozi waliokuwa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri  Tanzania  wakiuliza maswali na kutoa Maoni baada ya NSSF kuwasilisha mada katika mkutano huo
Baadhi ya viongozi na maafisa kutoka NSSF wakijibu maswali na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari baada ya semina kwa wahariri. Jukwaa la Wahariri waliandaa mkutano wao wa mwaka uliofanyika Zanzibar. NSSF ni mojawapo ya wadhamini wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa  Jukwaa la Wahariri  Tanzania na wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad