Afisa
Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA Winnington Makaka akitoa elimu kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule
ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za
Bodi ya NBAA.
Mkaguzi
wa ndani wa NBAA, CPA George Lazaro akitoa elimu kuhusu kazi za wakaguzi
kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaosoma masomo ya Biashara katika
Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika
ofisi za Bodi ya NBAA.
Na Mwandishi Wetu
Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea
kutoa elimu/mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi, Vyuo pamoja na Shule za
Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli
mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.
Akizungumza
wakati wa kutoa mafunzo hayo Mdhibiti wa Viwango wa NBAA, CPA
Winnington Makaka amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya
kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa
cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya
kazi nje na ndani ya nchi.
Aliongeza
kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu
nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya
ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya
Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza
kufanya mitihani ya Bodi alisema Makaka.
Naye Mkaguzi
wa ndani wa NBAA CPA George Lazaro ametoa elimu kuhusu tofauti iliyopo kati ya Mkaguzi na Mhasibu na kuainisha kazi za wakaguzi
kwa wanafunzi wa Kidato cha sita wanaosoma masomo ya Biashara katika
Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea ofisi za Bodi ya NBAA Dar es Salaam ili kujifunza juu ya Taaluma hiyo.
Akiishukuru
Bodi hiyo, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas
Mahundi amesema Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania
(NBAA) imetoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa wanaosoma masomo
ya biashara katika shule hiyo na elimu hiyo iliyotolewa itawasaidia
wanafunzi wa Baobab katika masomo yao na kwa hapo baadae.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara
katika Shule ya Sekondari ya Baobab wakifuatilia mada kwa wataalam
kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
walipotembelea ofisi za Bodi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment