HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 18, 2022

MKAZI WA CHANIKA NURU MIKIDADI AIBUKA NA KITITA CHA MILIONI KUMI KUTOKA BIKO

 
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.


Mwanadada mdogo kabisa mwenye umri wa miaka 20 tu, Nuru Mikidadi mwenye maskani yake Chanika, jijini Dar es Salaam, ameingia kwenye ulimwengu wa mamilionea wa bahati nasibu ya biko, baada ya kushinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa iliyofanyika Jumapili iliyopita.

Nuru amekabidhiwa fedha zake jana jijini Dar es Salaam, akiitumia fursa nzuri ya kucheza biko kwa kutumia namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456, bila kusahau wanaocheza kwa kuingia mtandaoni kwa www.biko.co.tz.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Nuru aliishukuru Biko kwa kumpa fedha zake mapema, huku akiwashauri Watanzania wote kuchangamkia fursa ya bahati nasibu hiyo ya Watanzania wote ili nao wafanikiwe kushinda kama ilivyokuwa kwake kwenye droo kubwa pamoja na wanaoshinda papo kwa hapo kuanzia sh 2500 hadi milioni tano kila sekunde moja.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

Mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam, Nuru Mikidadi, akifurahia pesa zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko droo iliyofanyika Jumapili iliyopita. Makabidhiano ya fedha zake yalifanyika katika benk ya CRDB, Tawi la Premier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu.Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kushoto akifurahia tukio la kumkabidhi Nuru Mikikadi (katikati) Sh Milioni 10 zake alizoshinda kwenye droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Biko iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Kulia ni Flamiana Msilu, Meneja Uhusiano wa CRDB Tawi la Premier lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad