MAKONDA AUNGA MKONO UCHUNGUZI JESHI LA POLISI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 12, 2022

MAKONDA AUNGA MKONO UCHUNGUZI JESHI LA POLISI

Na Humphrey Shao,Michuzi Tv

Baada ya CCM kutaka kuundwa kwa kamati ya kulichunguza Jeshi La Polisi kufuatia malalamiko mengi ya Watanzania, Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda , ameibuka Katika ukurasa wake wa Instagram na kusema yupo tayari kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo.

Makonda ambaye kuwa kimya Kwa muda mrefu huku akiandamwa na mzimu wa kutaka ashtakiwe leo ameamua kuvunja ukimya Kwa kuandika juu ya uonevu unaofanywa na Jeshi la Polisi.

"Naunga mkono hoja ya kamati kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi, wanaolipaka tope jeshi la polisi kwakuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi PAUL MAKONDA niko tayari kutoa ushirikiano" ameandika Makonda .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad