Afisa
Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya Nmb, Filbert Mponzi (wa
tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha Droo ya mwisho ya
msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako. Kutoka kushoto
ni Meneja NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, Mkuu wa Idara ya
Wateja Binafsi Benki ya NMB, Aikansia Muro na Mwakilishi kutoka Bodi ya
Michezo ya kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga, (kulia) ni Meneja
Mwandamizi kitengo cha Kadi, Manfredy Kayala na Balozi wa Kampeni hiyo,
Masoud Kipanya.
**********************
MIEZI mitatu ya
Kampeni ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ iliyoendeshwa na Benki ya
NMB, imefikia tamati leo kwa wateja 30 kujinyakulia kitita cha Sh. Mil.
90 (sawa na Mil. 3 kila mmoja), hivyo kukamilisha kinyang’anyiro
kilichobeba zawadi ya pesa taslimu Sh. Mil. 240.
Hitimisho
‘Grand Finale’ la kampeni hiyo, limefanyika NMB Tawi la Sinza jijini Dar
es Salaam, kufikia ukomo kwa mchakato uliowanufaisha wateja 1,080, kati
yao 1,000 wakijinyakulia Sh. Milioni 100 (sawa na Sh. 100,000 kila
mmoja), huku 50 wakitwaa Sh. Mil. 50 (sawa na Mil. 1 kila mmoja) na 30
wa fainali wakishinda Mil. 90 hizo.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi
na Biashara, Filbert Mponzi, alisema malengo ya kampeni hiyo, ambayo ni
kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, yamefanikiwa kwa
kiasi kikubwa na kumekuwa na ongezeko la asilimia 10 ya watumiaji wa
kadi.
Huu sio mwisho, kampeni hizi zitaendelea na tutaendelea
kutoa elimu kwa jamii itambue umuhimu wa kutumia kadi badala ya pesa
taslimu, kwa sababu ni rahisi, nafuu na salama zaidi.
Thursday, March 24, 2022

KISHINDO FAINALI NMB MASTABATA, MIL. 90/- KWA WASHINDI 30.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment