HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 22, 2022

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu wakiwemo wa matukio ya mauaji.

 

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUAJI
Mnamo tarehe 21.03.2022 majira ya saa 17:00 jioni, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Songwe lilifanya msako huko Kijiji cha Mwaka - Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa EMMANUEL PATSON MWESA [22] Mkazi wa Mwaka – Tunduma aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la mauaji ya bosi wake aitwaye ASUMWISYE LUFINGO @ MWAMBONIKE [37] Mkazi wa Isangawana tukio lililotokea mnamo tarehe 02.01.2022 wakiwa shambani.

Ni kwamba mnamo tarehe 02.01.2022 majira ya saa 16:00 mchana huko Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, ASUMWISYE LUFINGO @ MWAMBONIKE [37] akiwa shambani na vibalia wake mtuhumiwa EMMANUEL PATSON MWESA [22] na mwenzake aliuawa kwa kukatwa panga kichwani. Chanzo cha tukio ni madai ya fedha ya ujira ya kulima shamba. Aidha katika tukio hilo, watuhumiwa waliondoka na Pikipiki ya marehemu yenye namba za usajili MC.776 BES aina ya Fekon.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza msako na hatimaye kumkamata mtuhumiwa huko mkoani Songwe. Aidha Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa mwingine ambaye walishirikiana katika tukio hili. Aidha mahojiano na mtuhumiwa yanaendelea ili kubaini ilipo Pikipiki ya marehemu waliyoondoka nayo mara baada ya kufanya tukio hilo.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUAJI
Mnamo tarehe 20.03.2022 majira ya saa 13:30 mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kijiji cha Shitete, Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya na katika msako huo tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa SAFARI ADMIN LUWOLE [43] Mkazi wa Kijiji cha Horongo aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la mauaji ya mke wake aitwaye TUMAIN ANTHON [45] tukio lililotokea tarehe 04.02.2022.

Ni kwamba mnamo tarehe 04.02.2022 majira ya saa 07:00 asubuhi huko Kijiji cha Inolo, Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya, TUMAINI ANTHON [45] Mkazi wa Inolo alikutwa ndani ya nyumba yake akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa kitu Kizito kwenye paji la uso na mume wake aitwaye SAFARI ADMIN LUWOLE [43] Mkazi wa Kijiji cha Horongo. Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia kati ya marehemu na mumewe (mtuhumiwa).

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza msako mara moja na mnamo tarehe 20.03.2022 tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MATUKIO YA WIZI.
Mnamo tarehe 20.03.2022 majira ya saa 12:00 mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kijiji na Kata ya Ubaruku, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya na katika msako huo tulifanikiwa kumkamata LUCY ANTHONY MWALONGO [20] Mkazi wa Ubaruku akiwa na mali mbalimbali za wizi nyumbani kwake ambazo ni:-

1. Vyombo vinavyotumika majumbani vya aina mbalimbali,
2. Nguo aina mbalimbali,
3. Kadi ya benki,
4. TV aina ya Aborder inch 19,
5. Radio aina ya aborder,
6. Speaker 02,
7. Simu Smartphone 02 aina ya Tecno,

8. Plag socket 01, vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Tsh. 900,000/=. Mali zote zimetambuliwa na mhanga aitwaye RAPHAEL EDWARD [34] Mkazi wa Ubaruku. Upelelezi wa shauri hii unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad