HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 8, 2022

DAWASA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

 

DAWASA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Tarehe 8 Machi kila mwaka ni siku ya Wanawake duniani ambapo siku hii inakumbusha na kutafakari juu ya matokeo ya Kijamii, Kisasa na Kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Katika kuadhimisha siku hiyo wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya uhuru mkoani Dar es salaam huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni kizazi cha Haki na ustawi kwa maendeleo endelevu

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani DAWASA, CPA Rosemary Lyamuya amesema kuwa DAWASA inaadhimisha siku hii kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwani *amewatua ndoo za maji* Wanawake wa Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.

"Sisi kama Watumishi wanawake wa DAWASA tunampongeza Rais Samia Suluhu kwani maadhimisho haya yamekuwa ya mafanikio makubwa sana kwetu kwani utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Majisafi imewezesha kumtua mwanamke ndoo ya maji. Tumemtua mwanamke ndoo ya Maji maeneo mbalimbali kwa kukamilisha miradi ya Maji katika maeneo ya Kisarawe, Pugu, Chalinze, Mkuranga, Mbwawa ambayo kwa kiasi kikubwa imemuondolea mwanamke changamoto ya upatikanaji huduma."Alisema Rosemary
Ameongezea kuwa mafanikio yoyotr yanayoonekana hapa Nchini na Dunian lote kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na uwepo wa Wanawake katika nyadhifa kubwa na muhimu za kimaamuzi chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu.
Baadhi ya Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakipita kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Hassan Rugwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo March 08, 2022 katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duninia yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad