WAKULIMA NZEGA WAPO TAYARI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 23, 2022

WAKULIMA NZEGA WAPO TAYARI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO

 

Na Mwandishi wetu  - Nzega

Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora, wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa silimia mia.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na ukarabati wa miundombi katika skimu hiyo utasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua, tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.

“Naamini kuwa baada ya ujenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi .” Alisee Mkulima hiyo.

Akiongea wakati wa makabithiano hayo, Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema, eneo la skmu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa  Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga lenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo, lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.

Aliendelea kusema kuwa, awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane, utaboresha miundombinu na kusaidia wakulima  kuwa na kilimo cha uhakika.

 Mhandisi Mwinchuma Tengeneza (kulia) akimkabidhi kablasha la eneo la kazi ya  Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main Constructors Ltd Bw. Basil Clement (kushoto).

Wa pili kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Idudumo Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa neo la mradi
Sehemu ya eneo la Bwawa Idudumo, ambalo litafanyiwa ukarabati katika awamu nyingine ya mradi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad