TAASISI YA MARIAM MWINYI YAKABIDHIWA MASHINE 10 ZA MWANI NA BENKI YA NBC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 21, 2022

TAASISI YA MARIAM MWINYI YAKABIDHIWA MASHINE 10 ZA MWANI NA BENKI YA NBC


Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mariam Mwinyi amezindua Taasisi yake ya Zanzibar Maisha Bora kwa Wanawake, Vijana na Watoto na kukabidhiwa mashine 10 za kuchakata zao la Mwani kutoka Benki ya NBC.

Kabla ya Uzinduzi huo, Mke wa Rais aliweza kuongoza matembezi ya Km 6 kutoka Viwanja vya Butrous Kiembe Samaki hadi Uwanja wa Mao Ze Dong.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo, Mama Mwinyi amesema asilimia themanini(80) wanaojihusisha na kilimo cha zao la mwani ni wanawake ambapo wengi wao wanaishi maeneo ya Pembezoni mwa bahari.

“Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora inalenga kusaidia wanawake hao kunufaika na uchumi wa Buluu kupitia zao la mwani na tutashirikiana na serikali pamoja na wadau kuongeza uzalishaji bora, thamani na masoko ya zao hilo ili wanawake walio katika sekta hiyo waifanye kwa ufanisi na kuwaletea tija,” amesema Mama Mwinyi

Amesema, “Ninatoa ahadi ya kukabidhi mashine 16 kwa Vikundi 8 vya wakina mama vinavyojishughulisha na zao la Mwani kwa Pemba na Unguja, na kutakuwa na programu za kuwapatia ujuzi na vifaa,”

Mama Mwinyi, aliweza kutembelea Banda la NBC na kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya hiyo sambamba na Huruma ya Mobile Clinic ambayo inapatikana nchi nzima.

Pia, ameishukuru Benki ya NBC kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kuhakikisha Taasisi ya Zanzibar na Maisha Bota inawainua Wanawake na Vijana kupitia Uchumi wa Buluu( bahari).

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC, Meneja wa Tawi la NBC Unguja Ramadhan Lesso amesema Benki ya Taifa ya Biashara itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora na kuona umuhimu wa kushirikishwa na watakabidhi Mashine 10 za kuchakata Mwani.

“Mashine hizi zitasaidia kuwainua akina mama kuchakata mazao yao ya Mwani na kutengeneza bidhaa zao kutumia malighafi hiyo na uzuri ni kuwa Mashine zimetengenezwa na wazanzibar wenyewe,”amesema

“Tutaendelea kushirikiana na Taasisi ya Mama yetu Mariami Mwinyi katika kuinua Uchumi kwa wanawake, vijana na watoto ndani ya Zanzibar na kuwasihi wazanzibar wote kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora,”

Amesema, mashine hizo zimekabidhiwa kwa Taasisi hiyo na NBC imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Wanashirikiana na taasisi mbalimbali kupambana na umaskini.

Mashine hiyo imekabidhiwa wakati wa Uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika mapema Katika Uwanja wa Mao Ze Dong jana Visiwani Zanzibar.

Mwani ni moja ya mazao ya baharini yanayolimwa sana Visiwani Zanzibar na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora imeweka mkakati wa kuwainua wakina mama na vijana kupitia uchumi wa Buluu.

Mbali na kukabidhi mashine hizo, NBC walikabidhi pia mfano wa hundi ya Milioni 23 kwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mariam Mwinyi.

Benki ya NBC kwa mwaka 2022 imeweka kiasi cha Bilioni 100 katika sekta ya Kilimo ili kusaidia wakulima wa mazao mbalimbali.

Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar Ramadhan Lesso akimkabidhi Mfano wa Hundi ya shilling milioni 23 kwa Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Na Mwanzilishi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mariam Mwinyi wakati wa Uzinduzi wa Taasisi hiyo ulioenda sambamba na Kukabidhiwa mashine 10 za kuchakata zao la mwani. Uzinduzi huo umefanyika Katika viwanja vya Mao Ze Dong Visiwani Zanzibar
Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Na Mwanzilishi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mariam Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Meneja Maendeleo Biashara Tawi la Benki ya NBC Zanzibar Obedy Ngavatula baada ya Kutembelea Huduma ya Mobile Clinic inayotolewa na Benki ya NBC nchi nzima, Mariam Mwinyi amefanya uzinduzi wa Taasisi yake ya Zanzibar Maisha Bora yenye lengo la kusaidia wanawake, vijana na watoto
Wake wa Viongozi waliopo madarakani na waliostaafu wakipata maelezo kutoka kwa muhudumu wa Gari la kuhudumia wagonjwa la Mobile Clinic wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ya Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mariam Mwinyi iliyofanyika mwishoni ,wa wiki hii katika Viwanja vya Mao Ze Dong Visiwani Zanzibar.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Ramadhani Lesso akitoa maelezo kwa Askari Polisi aliyefika katika banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ya Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mariam Mwinyi iliyofanyika mwishoni ,wa wiki hii katika Viwanja vya Mao Ze Dong Visiwani Zanzibar.
Wateja wa NBC wakiendelea kupata huduma katika Banda lao
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad