HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 25, 2022

SERIKALI YA TANZANIA KUIMARISHA UHUSIANO NA WADAU WA MAENDELEO.


Serikali ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano baina yake na Mfuko wa Kimataifa wakusaidia mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria unaoitwa (The Global Fund) katika kuhakikisha afya za wananchi zinaimarika na wananchi kufanya shughuli zao katika mazingira salama.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Paul Sangawe wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau hao Jijini Dodoma.

Mkurugenzi amefafanua kwamba lengo la kukutana na wajumbe hao ni kuweka mikakati thabiti ya kuimarishaji mapambano dhidi ya magonjwa hayo pamoja na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara na taasisi zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na mfuko huo.

Aidha viongozi na wadau hao wamekutana na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni Ofisi yenye wajibu wa Uratibu wa utekelezaji wa programu ya Global Fund na shirika muhimu sana linaloleta tija katika utekelezaji wa miradi.

Aidha jukumu lingine la Ofisi ya Waziri Mkuu ni kufuatilia fedha zote zinazotolewa na wafadhili na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa pamoja na kuhimiza wadau kutumia fedha hizo kwa  wakati huku akieleza kwamba ipo haja ya kusimamia vyema misaada inayotolewa kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

“Tumejadiliana pia kuhakikisha tunaelekeza fedha zote za miradi kila baada ya miaka mitatu na kuangalia uwekezano wa kuzalisha baadhi ya vifaa tendanishi  ambavyo kwa sasa vinaagizwa kutoka nje kwa hiyo tutaangalia kwa namna gani misaada inayotolewa inatumika kwa ufanisi na  kuleta tija kwaTaifa letu si tu kuzalishwa ndani pia na kutoa ajira,” alieleza Sangawe.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afrika wa Global Fund Bw. Linden Morrison alishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuhakikisha  wanapambana na magonjwa mbalimbali ili wananchi wake kuwa na afya bora.

“Serikali ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya magonjwa mbalimbali kwa sababu wananchi hawawezi kufanya shughuli za uzalishaji ikiwa hawana afya bora na  katika hili na sisi kama Global Fund tuko tayari kushirikiana na Tanzania,” alipongeza Bw.Morisson.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akizungumza katika kikao  na Mkuu wa Idara ya Afrika Global Fund Bwn. Linden Morrison pamoja na ujumbe wake katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome –Dodoma hii leo Februari 24, 2022.
Mkuu wa Idara ya Afrika Global Fund Bw. Linden Morrison akizungumza katika kikao na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu Shughuli za serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Sera bunge na Uratibu katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome-Dodoma.
Katibu Mtendaji wa TNCM, Dkt. Rachel Makunde akichangia jambo katika kikao mbele ya Ujumbe kutoka Global Fund uliongozwa na Mkuu wa Idara ya Afrika Globa Fund.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad