Meridianbet
wameshirikiana na Polisi, kituo cha Mtongani Police Post Kuboresha
muonekano wa kituo hicho kwa kupaka rangi, ikiwa ni moja ya jitihada zao
za kurejesha kwa Jamii.
Kampuni ya Meridianbet, ambayo ni
Kampuni kongwe zaidi ya ubashiri Tanzania, ambayo ina masoko mengi ya
Ubashiri imekuwa ikishiriki shughuli mbali mbali za kijamii. Ikiwa ni
pamoja na kutembelea vituo vya wagonjwa na watu wenye mahitaji maalumu
ili kuwashika mkono.
Kwa mujibu wa Afisa kutoka kitengo cha
Masoko wa Meridianbet, Twaha Mohamed, Meridianbet wanaendelea kujiweka
Karibu zaidi na umma wakiamini usalama wa umma na wateja wao ni jambo la
msingi, muonekano mzuri wa kituo cha polisi ni muhimu wakati wao
wakishughulikia usalama wa raia na mali zao.
“Ndiyo, sisi kwa
upande wetu tumepata hamasa ya kufanya hili, kama ambavyo tunafanya
shughuli zingine za kijamii. Kupaka rangi kituo cha polisi ambao
wanahusika moja kwa moja na ulinzi wa raia na mali zao ni moja ya
shughuli za kuwa Karibu zaidi na Jamii na kuboresha uhusiano na Jamii na
wateja wetu.”
Uupande wa polisi, Mkuu wa kituo cha Mtongani,
ametoa shukrani zake na kutoa wito kwa makampuni mengine kushirikiana na
Jamii kwa mfano wa Meridianbet.
Meridianbet wanaahidi kuwa
wataendelea kushirikiana na jamii, na wana mipango ya kuhakikisha
wanakuwa bega kwa bega na jamii katika nyakati zote na nyakati za
matatizo.
“Tunaendelea kujitahidi kuwa Karibu sana na Jamii
yetu, maana ndiyo wateja wetu walipo na uhalisia pia kuwa tunatakiwa
kuwajibika kwa Jamii. Meridianbet katika msoko yake duniani kwote
tunafanya jitihada za kuwa Karibu na umma hata wakati wa matatizo kama
tulivyojitahidi kwa nafasi yetu mwanzoni mwa covid-19”
Meridianbet
wametaja kuwa zoezi hilo lilienda sambamba na uboreshaji wa maduka yao
katika eneo la Mtongani, kuwafanya wateja wapate huduma bora zaidi za
ubashiri kwa michezo ya kasino na bashiri za michezo.
Tuesday, February 22, 2022
Meridianbet Wachangia Uboreshaji Kituo Cha Polisi Mtongani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment