MAHAFALI YA WAHITIMU WA NDEGE NYUKI "DRONE" KWA KUTUMIA WATAALAM WA NDANI YAFANYIKA CATC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 11, 2022

MAHAFALI YA WAHITIMU WA NDEGE NYUKI "DRONE" KWA KUTUMIA WATAALAM WA NDANI YAFANYIKA CATC

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga    (katikati  ) akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari  wakati wa hafla ya kuwatunuku   vyeti wahitimu wa  Mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’   yanayotolewa na  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kutumia wataalam wa ndani
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), John Ndimbo akizungumzia namna walivyoweza kutoa mafunzo kwa kutumia wataalam wa ndani waliofanikisha watahiniwa wa mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ kusoma bila tatizo lolote na kuhitimishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga  aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TCAA Hamza Johari .
Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya  uendeshaji Ndege nyuki ‘Drone’ wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wataalam wa ndani yaliyoanza kufanyika toka tarehe 17 Januari hadi tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2022 yanayotolewa na  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) wakati wa hafla ya mahafali ya wanafunzi hao yaliyofanyika TCAA jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga    (Kulia) akiwatunuku wahitimu wa mafunzo ya urubani wa Ndege nyuki (Drone) wakati wa mahafali yaliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Daniel Malanga   akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya urubani wa Ndege nyuki (Drone)  wakati wa mahafali ya sita na mahafali ya kwanza kwa kutumia wakufunzi wa ndani yaliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)  TCAA jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad