BALOZI WA TANZANIA NCHINI DRC ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 1, 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI DRC ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akisamiliana na Balozi wa Tanzania Nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Balozi Said Juma Mshana aliyemtembelea leo ofisini kwake, kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akimtambulisha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa (kushoto) kwa Balozi wa Tanzania Nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Balozi Said Juma Mshana (wa pili kulia) pamoja na  Balozi Mdogo wa Tanzania - Lubumbashi, Celestine Kakele (kushoto) wakati walipotembekea Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es salaam. Benki ya CRDB inatarajia kufungua kampuni tanzu  nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo hivi karibuni. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Balozi Said Juma Mshana aliyemtembelea leo ofisini kwake, kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Balozi Said Juma Mshana (kushoto), Balozi Mdogo wa Tanzania - Lubumbashi, Celestine Kakele (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi jipya la nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Jesca Nyachiro (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa (kulia) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi jipya la nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Wema Mwamunyange.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad