HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 20, 2022

WATENDAJI HALMASHAURI YA MKURANGA WAASWA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA WELEDI

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mwantumu Mgonja akionesha mfano kwa kupanda kwenye bodaboda alizokabidhi kwa Watendaji Kata leo Januari  18,2022 mkoani Pwani. 
Baadhi ya watendaji waliokabidhiwa pikipiki na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mwantumu Mgonja leo Januari  18,2022 mkoani Pwani. 

Na Khadija Kalili, Mkuranga
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani imewataka Watendaji Kata kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi katika kuwatumikia wananchi kwa haki ili waweze kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mwantumu Mgonja alipokuwa akikabidhi vitendendea kazi kwa Watendaji Kata ndani ya Halmashauri kwenye hafla fupi makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi za Halmashauri.

"Mkuranga yenye Kata 25 na Vijiji 125 imekua ikitumia mapato yake ya ndani katika kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kusaidia manunuzi ya vitendea kazi kwa watumishi wake ili kuweza kurahisisha utendaji wa kazi zao za kila siku kwa wananchi" amesema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Mkuranga Mwantumu

"Ninawakabidhi hizi pikipiki mkazitumie kama ni nyenzo kuu kwenu katika kazi na siyo vinginevyo na hasa kuwahi kufika katika Ofisi zenu kazingatieni kuwahi kufika kwa wakati na mkawatumikie wananchi kwa weledi wa hali ya juu binafsi nitawapitia katika ofisi zenu na kuwafuatilia namna mnavyowatumikia wananchi" amesema Mkurugenzi huyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Mohammed Mwera amesema ni lazima Watendaji wakwatumikie wananchi kwa sababu Halmashauri hiyo imelenga kuboresha mioundombinu mbalimbali sanjari na kuwatumikia vema wananchi wao.

Akizungumza kwa niaba ya Watendaji wenzake waliopewa vitendeakazi hivyo Mwenyekiti wa Watendaji Shaaban Mponda amesema kuwa wanamshuku sana Mkurugenzi wa Mkuranga kwa kuwajali na kuwarahisishia utendaji wao katika kazi hivyo wamemuahidi watafanya kazi kwa waledi na utii wa nidhamu kazini na kuwatumikia wananchi katika maeneo husika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad