HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 18, 2022

TARURA, MANISPAA KIGAMBONI WAJADILI RASIMU YA BAJETI YA MATENGENEZO YA BARABARA 2022/2023

 



Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Almas Nyangasa akizungumza na Madiwani na watendaji wa TARURA wakati akizindua kikao maalumu cha mapitio ya rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara katika Wilaya hiyo na kuwataka Madiwani hao kubainisha maeneo ya kimkakati ili yaweze kupata huduma ya barabara kwa haraka. Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Eng. Mussa Mzimbiri (katikati,) akifuatilia mjadala katika kikao hicho maalumu cha kujadili rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa Wilaya ya Kigamboni.




WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA,) wameendelea kushirikiana na Madiwani katika upitiaji ya rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka 2022/2023 katika Wilaya za jiji Dar es Saalam huku wakiahidi kusimamia matengenezo na ukarabati wa barabara pamoja na kuhakikisha kila Kata inafikiwa na mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami.

Akizungumza leo jijini Dar es Saalam wakati wa upitiaji wa rasimu ya utengenezaji wa barabara kwa Wilaya ya Kigamboni Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Eng. Mussa Mzimbiri amesema lengo na kushirikiana na baraza la Madiwani ni kutokana na  ukaribu wao na wananchi na wanajua mahitaji ya wananchi hasa kwa kubainisha maeneo yenye uhitaji zaidi.

Mzimbiri amesema kuwa, jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara za Wilaya hiyo na hazitatosha kwa mara moja katrika matengenezo hayo na kupitia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kupitia ofisi ya Mkurugenzi fedha za ziada zitakazoongezwa zitatumika kukarabati mtandao wa barabara wa Wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa kufukua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi. Fatma Nyangasa amesema, ushirikiano  uliopo baiana ya Wakala hiyo na baraza la Madiwani ni muhimu hasa katika uboreshaji wa mtandao wa barabara kwa kila Kata.

''Madiwani ni wawakilishi wa wananchi na wanajua maeneo yenye uhitaji zaidi...na fedha hizi hazitoshi kwa kufanya matengenezo ya pamoja niwaombe waheshimiwa Madiwani tuangalie zaidi maeneo ya kimkakati na kuhakikisha maeneo mengine yote yanapitika.'' Amesema.

Bi. Fatma amesema kuwa Wilaya hiyo ina mtandao wa barabara wenye kilomita 1035.39 na kati ya hizo kilomita 4.87 ni za kiwango cha lami, kilomita 323.85 kiwango cha changarawe na kilomita 706.67 ni za kiwango cha udongo.

Amesema uboreshaji wa barabara hizo kwa mwaka uliopita ulilenga kupunguza msongamano wa magari, kuwa na mawasiliano kuelekea katikaa maeneo yanayotoa huduma muhimu ikiwemo hospitali.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema Omary Ramadhani amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua miradi mingi ya maendeleo ikiwemo katika sekta za elimu, afya na miundombinu ya barabara na ameishukuru TARURA kwa kuwashirikisha katika miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara katika Wilaya hiyo.



Mijadala ikiendelea.




Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kikao hicho.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad