HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 27, 2022

NIT WAASWA KUZALISHA WATAALAMU KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI, UCHUKUZI

SERIKALI imekiasa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kuendelea kuzalisha wataalamu wengi zaidi katika sekta ya usafirishaji na Uchukuzi watakaosaidia kuendesha miradi inayofanywa na serikali ili kukuza uchumi wa nchi.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema hayo leo Januari 26,2022 wakati wa ziara yake chuoni hapo  na kujifunza mambo mbalimbali.

Amesema,  chuo cha Usafirishaji ni muhimu kwa uchumi wa Taifa ambo unategemea usafirishaji na Uchukuzi, hivyo ni ndoto kubwa kwa wizara yake kuona wataalamu wa sekta hiyo wanatoka hapa nchini.

"Nikiwa chuoni hapa nimejionea vitu vingi ikiwemo mifumo itakayotumika kiwafundishia  marubani,  ukaguzi wa gari shughuli nyinginezo jambo ambalo ni hatua kubwa kwa nchi" amesema Mwakibete.

Aidha amewashauri wasafirishaji na wamiliki wa vyombo vya moto kunitumia Chuo hicho kwa kujifunza ilk kuweza kuepuka ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikua wananchi wengi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zakaria Mganilwa amesema, chuo kitaendelea Chuo wataalamu katika nyanja zote za sekta hiyo kwani jukumu lao kubwa walilopewa na serikali kufundisha wataalamu watakaosaidia kuendesha miradi ya inayofanywa na serikali.

 Amesema, Serikali imefufua Shirika la ndege ATCL, na inajenga reli ya kisasa hivyo kwa kuangalia hayo sasa wako katika hatua ya mwisho ya kukamilisha mchakato wa kufundisha kozi ya urubani wa ndege kwa garama nafuu ya shilling milioni 70.

Amesema kuwa kati ya fedha hizo Sh21 milioni ni gharama za kozi hiyo ngazi ya awali ambayo itamuwezesha mwanafunzi kusoma masomo ya awali na kuruka angani saa 50.

Amesema ingawa bado hawajapata ndege za mafunzo ila wanatarajia muda siyo mrefu watapata ndege hizo ili waweze kuanza kuzalisha wataalamu kwa mtandao wote wa sekta ya anga.

"Chuo hiki kumekuwa kikitoa mchango mkubwa wa kukuza uchumi nchini kwa kuzalisha rasilimali watu sahihi kwa ajili ya sekta nzima ya uzalishaji na Uchukuzi.
Ameongeza kuwa, chuo pia kimepata eneo la ekari 1000 jijini Dodoma karibu na uwanja wa ndege wa Msalato ambalo watalitumia  kwa ajili ya kutengeneza mabehewa.

"Eneo letu hapa ni dogo ndio maana tumetafuta eneo hili kama tulivyotafuta eneo mkoani Mtwara lengo kuu likiwa kutanua wigo wa huduma zetu",amesema Profesa Mganilwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kumaliza kutembelea Kituo cha Kupima Magari kilichopo katika Chuo cha Taifa {NIT} wakati wa ziara yake  katika chuo hicho, jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2022.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji {NIT}, Profesa Zacharia Mganilwa  akiomuonesha Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete baadhi ya maeneo ya chuo hicho, jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2022.









Matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji {NIT}jijini Dar es Salaam leo Januari 26, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad