Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Joseph Mkirikiti (aliyevaa kofia nyeusi) akitazama kituo cha kuchotea
maji ambacho hakifanyi kazi jana alipokagua zahanati ya kijiji cha
Fyengeleza Manispaa ya Sumbawanga na kuagiza wataalam wa Ruwasa
kukamilisha mradi huo ili wananchi wapate maji. Wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya.
Tanki la maji lenye
uwezo wa kuhifadhi lita 150,000 za maji lililokamilika katika mradi wa
waji wa kijiji cha Mponda Manispaa ya Sumbawanga chini ya usimamizi wa
RUWASA .Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Joseph Mkirikiti (aliyevaa shati la kitenge) akitazama tanki la maji
lililojengwa na RUWASA Sumbawanga kwa ajili ya mradi wa maji kijiji cha
Mponda ambapo watu zaidi ya 1800 watanufaika ambapo mradi huo umegharimu
shilingi Milioni 240.
Mkazi wa kijiji cha Fyengeleza Jacklina Masanja (mwenye mtoto kushoto)
akizungumza kushukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya
kijiji hicho jana wakati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti
(aliyevaa kofia nyeusi) alipotembelea kuona huduma kituoni hapo.
Meneja wa TARURA Sumbawanga Mhandisi Samson Kalesi (kushoto ) akitoa
maelezo ya ujenzi wa barabara ya lami ya Petrol Station- High Court
yenye urefu wa kilometa moja jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Joseph Mkirikiti ( aliyevaa kofia nyeusi) jana mjini Sumbawanga
No comments:
Post a Comment