CHALINZE YAPITISHA BIL.48.09 YAWEKA KIPAUMBELE KWA SEKTA ZA AFYA , ELIMU NA MIUNDOMBINU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 25, 2022

CHALINZE YAPITISHA BIL.48.09 YAWEKA KIPAUMBELE KWA SEKTA ZA AFYA , ELIMU NA MIUNDOMBINU

 Na Khadija Kalili, Chalinze

MKUTANO Maalumu wa bajeti ya mwaka 2022/2023 Halmashauri ya Chalinze umepitisha bajeti ya shilingi Bil.48.09 huku ikianisha baadhi ya vipaumbele walivyowekwa ni katika sekta ya elimu na afya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Rajab Hassan Mwinyikondo alisema hayo jana alipozungumza na Waandishi wa habari kuwa vipaumbele vilivyowekwa ni katika kuiwezesha sekta ya serikali kwa kugusa katika maeneo ya afya , elimu na miundombinu.

Alisema kuwa Mil.225 ni bajeti inayoendelea kwa ajili ya afya na elimu huku kila Kata itapatiwa kiasi cha Mil.15.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa matundu ya vyoo mashuleni kuwa unahitaji kiasi cha Mi.200 ambapo
watajenga matundu ya vyoo kwenye majengo mapya ya shule zote zilizojengwa ndani ya Halmashauri ya Chalinze.

"Mimi binafsi nakiri kuwa mpango huu wa bajeti unakwenda kutatua changamoto za papo kwa papo kwa wananchi wetu"alisema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Chalinze.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Possi alisema kuwa anawashukuru sana waheshimiwa Madiwani kwa kuipitisha bajeti yetu ya mwaka ujao.

"Tumepandisha bajeti yetu zaidi ya Bil.10.6. hadi kwenda kiasi cha Bil.13.7,tumepitisha Bil.48.09 hii ni bajeti yetu ya mwaka 2022/2023 ikiwa ni mapato yetu ya ndani,hivyo tumepandisha mishahara" alisema Possi.

Akizungumzia kuhusu vipaumbele vya Halmashauri ya Chalinze katika sekta ya maendeleo kuwa wamegusa katika sekta zote ambazo ni elimu ,afya, miundombinu huku akibainisha kuwa wametenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Msoga ambayo itatumia zaidi ya Mil.400.

Mkurugenzi Possi aliongeza kwa kusema kuwa Halmashauri imetenga fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati kwa sababu Chalinze wana tatizo la maegesho ya magari makubwa ambayo yamekua yakizaa hovyo hivyo wamejipanga kudhibiti hali hiyo wananadaa sehemu Maalumu ya maegesho ambayo itachangia katika ukusanyaji wa mapato ambayo kwa Sasa yanapotea.
"Tumetenga kiasi cha Sh.Mil.200 ambazo Mil.100 zitakwenda katika ujenzi wa soko la Lugoba na Msata ambazo zitakamilisha ujenzi na tayari soko la Bulingu limeshakamilika"alisema Mkurugenzi Possi.

Alisema kuwa tayari wameshaanzisha Kituo Cha Mabasi (Chalinze Bus Stand)ambayo tayari imeshaanza kazi huku wakinipanga kukamilisha ujenzi Ili iwe katika viwango vya kisasa na inayostahili kwa matumizi ya wananchi na kudhibiti ukusanyaji wa mapato kwa ujumla.

Wakati huohuo Mkurugenzi huyo amekiri kuwa kuna Wafanyakazi watatu wa Halmashauri ya Chalinze wanamshikilia kwa tuhuma za kuchezea maeneo ya ukusanyaji wa kodi huku akisisitiza kuwa bado ni tuhuma na suala hilo linafanywa
uchunguzi na endapo watabainika ama kukutwa na hatia watachukuliwa hatua zinazostahili.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Rajab Hassan Mwinyikondo akizungumza wakati wa kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 48.09 Chalinze Mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Rajabu Possi Mwenye miwani kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Rajab Hassan Mwinyikondo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad