WANAWAKE WAASWA KUBADILIKA KUACHA UTENGANO,BALI WAUNGANE KUJIINUA KIUCHUMI-GUNDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 14, 2021

WANAWAKE WAASWA KUBADILIKA KUACHA UTENGANO,BALI WAUNGANE KUJIINUA KIUCHUMI-GUNDA

 Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WANAWAKE wanaaswa kushirikiana katika vikundi ili kujiinua kiuchumi, na hatua hii imejionyesha kwenye kikundi cha Kuweka na Kukopa cha Umoja ni Nguvu , Kata ya Kikongo, Kibaha, Mkoa wa Pwani, ambapo hadi Sasa kimekusanya sh.milioni 29.

Licha ya hatua hiyo,penye mafanikio hapakosi changamoto , kikundi hicho kinahitaji kupata elimu ya Ujasiriamali hali inayotimiza ndoto yao ya kuongeza ujuzi katika ujasiliamali mbalimbali ili kujipatia kipato kikubwa.

Josephine Gunda ambae ni Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Ruvu akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi Mbunge Michael Mwakamo aliwapongeza, kwa umoja huo na kueleza umoja ni nguvu utengano Ni udhaifu.

"Wanawake wanatakiwa wasikate tamaa ,wengi unakuta vikoba na vikundi wanavyoanzisha vinakufa kutokana na kutoelewana ,kutokuwa maanani na umoja wao,Ila nyie kikundi cha Umoja ni nguvu mmeonyesha mfano kuwa kila kitu kinawezekana Kama mkiwa kitu kimoja"

Gunda aliwaasa wanawake ,kuacha tabia ya kukatishana tamaa na kuendekeza chuki na kusemana na badala yake waungene kwani wakiwa pamoja watanufaika kwa urahisi.

Awali katibu wa kikundi hicho, Halima Jongo alisema ,kikundi hicho kina wanachama 48, kati yao wanaume 16 wanawake 32 ambapo miaka miwili kimekusanya shilingi milioni 29.

"Penye mafanikio hapakosi changamoto, tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa elimu ya ujasiriamali kwa kuanzia ufugaji wetu wa kuku, mikopo, pia tunahitaji kuwezeshwa kumalizia jengo letu la ofisi," alieleza Halima.

Kikundi cha Umoja ni nguvu ,kimeanzishwa Novemba 18 mwaka 2014 kina malengo ya kujiinua kiuchumi, kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ambapo tayari imewafikia walengwa zaidi ya MIAMOJA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad