HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

Wahitimu wa TIA waaswa kuwa wabunifu na wenye weledi wa kufanya kazi

 

*Dkt.Momole ataja mafabikio ya Taasisi kwa wahitimu wenye ushindani wa soko la ajira

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
MHASIBU Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango Leonard Mkude amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kujiendeleza kielimu ndani ya ajira ili kwenda na kasi ya ukuaji wa katika kufanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuiletea nchi maendeleo.

Akizungumza Desemba 4 2021 kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo katika mahafali ya 19 ya chuo hicho amesema wanafunzi hao hawapaswi kubweteka na elimu aliyoipata, wanatakiwa kutambua kuwa wanakwenda kuwatumia wananchi pamoja katika sekta mbalimbali nchini hivyo ni wajibu wao kutanguliza weledi wa kazi ukiwa ni pamoja na kujiepusha na rushwa.

Akizungumza mbele ya wahitimu zaidi ya 7000 kwa kampasi mbili amesema, “ninawaasa wanafunzi mnaohitimu ngazi mbalimbali kwamba elimu mnayoipata iwe chachu ya kujiongezea maarifa. Msiwe wataalamu wasio na tija katika kuleta maendeleo.”

Amewataka kutumia elimu waliyoipata kujitafutia soko la ajira na kujiajiri pamoja kuwa wabunifu kutokana ushindani wa soko la ajira

“Soko lilopo la ajira ni dogo, ni vyema mkaelekeza mawazo yenu kwenye kujiajiri na si kuajiriwa.

Mkude amesemab Watakaobahatika kuajiriwa jitahidini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu na kujiepusha na rushwa kwani inashusha taaluma ambazo mmepata katika chuo hiko ” amesema.

“Mmetoka hapa kwa kuandaliwa kama wataalam hivyo msikiache kuitumikie elimu hiyo katika kuleta maendeleo ya nchi na kuwa bora zaidi katika soko la ajira.”

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Momole Kasambala amesema zaidi ya wahitimu 7000 ambao wametunikiwa taaluma ambapo chuo kimekuwa na mafanikio na kufanya kila nwaka kuongeza udahili wa kujiunga

Dkt.Kasambala amesema kuwa licha ya mafanikio hayo lakini Chuo kimejiimarisha katika kuhakikisha wahitinu wanakwenda kuwa mabalozi wa Taasisi.

Dkt. Momole amesema TIA itaendelea kuuhisha mitaala inayoendana na mahitaji ya kitaifa na kimataifa kama dira ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania inavyosema “Kuwa Taasisi inayotoa elimu yenye ubora katika biashara, huduma za utafiti na Ushauri barani Afrika.

“Nawapongeza Wahitimu wote mkalitumikie Taifa letu kwa tija na uzalendo.” Kaimu Alisisitiza Dkt.Momole Afisa Mtendaji Mkuu.
Mgeni Rasmi pamoja na meza yake wakiwa katika heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kufunguliwa kwa mahafali ya 19 ya TIA.
Baadhi wahadhiri na watendaji wa TIA katika mahafali ya 19.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Wakili Said Chiguma akizungumza katika mahafali kutokana ushauri na Taaisisi kufanyia kazi kwa kupata matokeo chanya katika Mahafali ya 19 ya Taasisi hiyo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dk.Momole Kasambala akizungumza kuhusiana na mahafali ya 19 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Kampasi ya Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango Leonard Mkude akizungumza wakati wa kufungua mahafali ya 19 ya Taasisi ya Uhasibu Tananzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika Kampasi ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya picha ya wahitimu wakiwa wamesimama

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad