HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 15, 2021

UONGOZI MPYA TANZANIA GIRL GUIDES WAAHIDI MAKUBWA

Kamishna Mkuu mpya wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA), Mary Richard akiapishwa na Kamishna wa TGGA, Wakili Victoria Mandari kushika wadhifa huo mara baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi katika mkutano huo.

 

Na Richard Mwaikenda

Mwanasheria Mary Richard amechaguliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association ,TGGA) katika mkutano Mkuu wa chama uliofanyika jijini Dar Dar es Salaam  Desemba 13, 2021.


Mary na viongozi wengine wapya wa vijana wa TGGA, Mwenyekiti Irene Jeremiah na Katibu Amenciatha Makoko waliapishwa na Kamishna wa chama hicho, Wakili Victoria Mandari.Viongozi hao watahudumu katika nafasi hizo kwa miaka mitatu.


Kamishna Mkuu mpya, Mary  amehidi kuendeleza mazuri yote ya uongozi uliopita kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa kufuata katiba ya chama hicho pamoja na kuwajengea uwezo vijana wa kike kujitambua na kufanya kazi kwa bidii kuliletea Taifa maendeleo na wao wenyewe. 


Viongozi wengine waliochaguliwa  ni Kamishna Mkuu Msaidizi, Florentina  Bernard na Makamu Mwenyekiti wa TGGA Taifa, Consolatha Shayo. Nafasi ya Mwenyekiti Taifa iko wazi baada ya kutopigiwa kura kutokana kutojitokeza wala kutoa udhuru katika mkutano huo.

Mwenyekiti mpya wa Vijana TGGA  Taifa, Irene Jeremiah akila kiapo.
Katibu Mkuu wa  Vijana Taifa wa TGGA, Amenciatha Makoko akila kiapo cha TGGA. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa TGGA, Anna Maembe akiongoza Mkutano Mkuu wa TGGA uliofanya uchaguzi wa viongozi wapya.
Kamishna Mkuu wa TGGA, Mary Richard akitoa shukrani kwa wanachama kwa kumchagua kwa kura nyingi na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitumikia TGGA.
Mary Richard ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, akipiga kura wakati wa uchaguzi uliowaweka madarakani.
Mwenyekiti mstaafu wa  Bodi ya Utendaji ya TGGA, Profesa Martha Qorro akipiga kura.
Kamishna Mkuu mstaafu wa TGGA, Symphorosa Hangi akipiga kura kuchagua uongozi mpya.

Mjumbe msataafu wa Bodi ya Udhamini  ya TGGA, Zakhia Megji akichangia hoja wakati wa uchaguzi
Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Temeke, Komba akiuliza swali
Matokeo ya uchaguzi huo yakitangazwa
Katibu Mkuu wa TGGA, Wintapa Luila akitoa pongezi  kwa uongozi  mpya na shukrani kwa uongozi uliopita kwa ushirikiano walioutoa.
Wanachama wakiwa katika mkutano huo.












 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad