TCAA yatoa msaada wa Vitanda katika Shule ya Sekondari ya Azania - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 6, 2021

TCAA yatoa msaada wa Vitanda katika Shule ya Sekondari ya Azania

 


Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa makabidhiano ya vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikagua vitanda vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Desemba 06, 2021. Kulia ni Meneja Ununuzi wa TCAA Bw. Yoswan Nyongera aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania Bw. Melisius D. Kayombo(wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu vitanda kwa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu  mara baada ya kupokea vitanda hivyo kutoka TCAA leo Desemba 06, 2021. Kulia ni Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akielezea namna Serikali inavyotambua mchango wa  TCAA kwa jamii mara baada ya Mamlaka hiyo kukabidi vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikabidhi Cheti kwa Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera kwa niaba ya Mamlaka hiyo kwa kujitoa kusaidia jamii hasa kwenye Shule mbalimbali hapa nchini.
Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kuendelea kurudisha kwa jamii hasa kwenye Shule mbalimbali za hapa nchini mara baada ya kukabidhi vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya vitanda vilivyokabidhiwa shule ya Sekondari Azania kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Meneja Mawasiliano na Uhusiano TCAA Bi. Salome Mallamia akitoa utambulisho kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Azania wakati wa kukabidhi msaada wa vitanda (double decker) 26 katika Shule hiyo


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad