TCAA YAADHIMISHA WIKI YA USAFIRI WA ANGA KWA KUTOA SEMINA KWA WATOTO NA KUTEMBELEA UWANJA WA NDEGE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 4, 2021

TCAA YAADHIMISHA WIKI YA USAFIRI WA ANGA KWA KUTOA SEMINA KWA WATOTO NA KUTEMBELEA UWANJA WA NDEGE

 

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani, Mamlaka imeendesha mafunzo Kwa watoto wa watumishi wa TCAA kuhusu Usafiri wa Anga na  kufanya ziara katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa semina hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga  amesema Mamlaka hiyo imeamua kuandaa semina ili kuweza kutoa elimu kwa watoto hao ili waweze kujua kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa nadharia pamoja na vitendo.

Pia amesema watoto ni taifa la kesho hivyo wanapaswa kuandaliwa vyema ili kuweza kufikia malengo pamoja na ndoto zao hivyo wanapaswa kusimamiwa kwa kupewa elimu iliyobora na yenye tija kwa maisha yake ya baadae.

Amesema elimu watakayoipata kwenye semina hiyo isiishie hapo bali iwe chachu kwao na wakawe mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa watoto wenzao wa mtaani pamoja na shuleni.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga  akizungumza na wanafunzi wa watoto wa watumishi wa TCAA waliofika kwenye semina ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Shukuru Nziku akitoa semina kwa watoto wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) waliofika kwenye Mamlaka hiyo ili kupata elimu ya kazi zizofanywa na mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Watoto wakiwa kwenye chumba cha kuongezea ndege kilichopo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Watoto wakiwa kwenye picha ya pamoja


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad