T-MARC TANZANIA WASHEREHEKEA SIKU YA UKIMWI DUNIANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 2, 2021

T-MARC TANZANIA WASHEREHEKEA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

 

 


Shirika lisilo la kiserikali, T-MARC Tanzania ambayo ni mshirika wa karibu wa serikali katika mapambano ya vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi imedhihirisha umahiri wake katika   maonyesho ya wiki moja ya siku ya Ukimwi duniani yaliyohitimishwa Jana katika  Uwanja wa Ruandansovwe, jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ilitotolewa na T-MARCK ilisema kuwa maonyesho hayo yalihitimishwa  kwa kusherehekea siku ya Ukimwi duniani ambayo kitaifa ikifanyika jijini hapa.
T-MARC Tanzania ilishiriki kwa kuwa na banda kwenye wiki ya maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yana kauli mbiu inayosema “Zingatia Usawa.Tokomeza Ukimwi. Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko” kutokana na kuwa mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika vita vya mapambano dhidi ya Ukimwi.
 
Katika maonyesho hayo banda la T-MARC lilionekana kuwa kivutio kutokana na namna ambavyo walionyesha umahiri katika shuguli zake za huduma za afya ikiwemo mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi, Kifua Kikuu, uzazi wa mpango, afya ya uzazi, lishe, Malaria, Maji na suala la usafi wa mazingira pamoja na kuhamasisha utoaji wa nafasi kwa mtoto wa kike katika maendeleo yake.
Katika elimu waliyokuwa wakitoa T-MARC wameweza kueleza bayana kuhusu njia inayotumiwa zaidi kupata maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni ya kujamiana ambayo huchangia kwa asilimia 80.

Katika week hii ya maonesho T-MARC imepeleka mafunzo ya kuhamasisha matumizi ya Kondom zao pendwa za  Dume Classic, Dume Desire, na Dume Extreme, ambazo zinalenga rika mbalimbali na watu wenye kipato tofautitofauti huku wakilenga vijana na watu walio kwenye sehemu hatarishi.
Hadi sasa T-MARC imeuza na kuzambaza kondom milioni 60 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Ikiwa kama kitovu cha utendaji uliotukuka, T-MARC Tanzania ina Jukumu ya kuhakikisha jamii inapata huduma za afya za kudumu na za uhakika kwa kushirikiana na washirika wake, na imekuwa ikifanya hivyo katika miaka inayokaribia 20.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad