SIMBA YAIFUATA RED ARROWS KWA TAHADHARI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 3, 2021

SIMBA YAIFUATA RED ARROWS KWA TAHADHARI

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
KIKOSI cha Simba kimeondoka leo kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mtoano wa Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Jumapili Desemba 05.

Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema wamejipanga vizuri kwa mchezo wa marudiano japo wanafahamu utakuwa ni mgumu kwao.

Pablo amesema anajua Red Arrows wanataka kupata matokeo katika Uwanja wao wa nyumbani, ila Simba wanamtaji wa mabao hivyo wamejipanga kuhakikisha wanalinda ushindi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere pamoja na kikosi wakiwa tayari kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo.

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu Red Arrows watataka kushinda lakini tumejipanga kupambana nao, kikubwa tunahitaji kulinda ushindi wetu tuliopata katika mchezo uliopita"amesema.

" Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu na tunafahamu kitu gani tunatakiwa kufanya kuelekea mchezo wa jumapili ili kuwapa furaha mashabiki wetu"amesema

Katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba walipata ushindi wa goli 3-0 na Red Arrows wanatakiwa kushinda goli 4-0 au na zaidi ili kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Simba walitolewa katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy na kupangiwa kucheza mchezo wa Play Off dhidi ya Red Arrows.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad