NSSF yaandikisha wanachama wapya katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru, Tanga - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 9, 2021

NSSF yaandikisha wanachama wapya katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru, Tanga

 


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Audrey Claudius (wapili kulia) kuhusu shughuli zinazofanywa na NSSF katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo kimkoa zinafanyika Wilaya ya Korogwe. NSSF ilitumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuandikisha wanachama wapya na kutatua kero mbalimbali.

Na MWANDISHI WETU

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulikuwa miongoni mwa Taasisi za Umma zilizoshiriki katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara mkoani Tanga ambazo kimkoa zilifanyika wilayani Korogwe.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima ambapo Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga,  Audrey Claudius alisema kupitia maadhimisho hayo Mfuko ulikuwa unatoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ambapo walifanikiwa kuandikisha wanachama wapya zaidi ya 50.Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulikuwa miongoni mwa Taasisi za Umma zilizoshiriki katika kilele cha Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo kimkoa yalifanyika  katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima. Pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Tanga walioshiriki uzinduzi huo.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad