NAIBU WAZIRI MWANAIDI AIAGIZA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUFANYA UTAFITI HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 3, 2021

NAIBU WAZIRI MWANAIDI AIAGIZA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUFANYA UTAFITI HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akitoa vyeti vya kufanya vizuri wanahitimu katika mahafali ya 45 ya taasisi ya ustawi wa jamii yaliyofanyika leo Desemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis amemuagiza Kamishna wa Ustawi wa Jamii kushirikiana na Menejimenti ya Taasisi hiyo kuainisha maeneo ya ushirikiano na kupanga mikakati ya pamoja ili kuwatumia wahitimu katika utoaji wa huduma za jamii, tafiti na ushauri wa kitaalamu.

Hayo yamesemwa na Mwanaidi Ally Khamis wakati wa Mahafali ya 45 ya taasisi ya ustawi wa jamii yaliyofanyika chuoni hap oleo Desemba 3, 2021 Amesema kuwa serikali inaiangalia taasisis hiyo kwa jicho la kipekee.

Amesema hatua hiyo ni kubwa katika kuimarisha uwezo wa Taasisi ambayo itawezesha kutoa wanafunzi waliobobea katika fani mbalimbali.

Amesema kuwa Katika hotuba ya Bajeti kwa mwaka 2021/2022, Wizara ya afya kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii iliainisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji ikiwemo kuwezesha mafunzo ya ufundi stadi, ujasiriamali na stadi za maisha kwa watoto wanaokinzana na sheria katika mahabusu za watoto na shule ya maadilisho.

Kuwezesha kuwaunganisha na familia zao watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika mikoa 26 nchini, Kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa wazee pamoja na upatikanaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kwa wazee katika makazi ya wazee nchini, Kuwezesha utungaji wa Sheria ya Taaluma ya Ustawi, Kufanya mapitio ya mwongozo wa huduma za malezi ya kambo na kuasili pamoja na Kufanya ufuatiliaji wa ubora wa huduma za Ustawi wa Jamii.

"Pia nimefurahishwa na jinsi mlivyoweka mkazo kwenye mafunzo ya vitendo ili kumpa mwanafunzi uzoefu na ujuzi wa ziada katika fani anayosomea. Hatua hii itapunguza ama kuondoa kabisa pengo lililopo kati ya mahitaji ya soko la ajira na uwezo wa wahitimu wetu. Alisema Naibu Waziri Mwanaidi.

Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewataka wahitimu hao kusimamia misingi na maadili ya taaluma mbalimbali walizojifunza kwenye Taasisi hiyo, pamoja na kuweka uzalendo na upendo kwa nchi yao.

Pia ameipongeza Menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia hasa kusomesha wahadhiri kwenye ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PHD).

Awali Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Joyce Nyoni amesema kwa mwaka wa masomo 2020/2021 katika mahafali hayo wahitimu 1,271 sawa na asilimia 68 ni wanawake na 596 ni wanaume, sawa na asilimia 32.

Hata hivyo amesema Taasisi inajivunia mafanikio iliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili kutoka wanafunzi 3,159 kwa mwaka wa masomo 2020/21 hadi 5,122 kwa mwaka wa masomo 2021/22.

"Pia imeendelea kuwasomesha walimu pamoja na wafanyakazi katika ngazi mbalimbali ili kukidhi mahitaji yetu na kuendana na kasi ya ongezeko la wanafunzi. Taasisi pia imeendelea kuboresha mitaala yake ili iendane na mahitaji ya soko na kujenga wahitimu wanaolenga katika kujiajiri," amesema Dkt. Nyoni.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wazazi pamoja na wahitimu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam leo Desemba 3,2021 katika mahafali ya 45 ya taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis katikati kulia ni  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara ya Maendeleo ya Jamii, Patrick Golwike  na kulia ni Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Joyce Nyoni 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akitoa vyeti vya kufanya vizuri wanahitimu katika mahafali ya 45 ya taasisi ya ustawi wa jamii yaliyofanyika leo Desemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akitoa vyeti vya kufanya vizuri wanahitimu katika mahafali ya 45 ya taasisi ya ustawi wa jamii yaliyofanyika leo Desemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahitimu wakiwa katika mahafali ya 45 ya taasisi ya ustawi wa jamii leo Desemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.

Wahitimu wakiingia katika mahafali ya 45 ya taasisis ya Ustawi wa Jamii leo Desemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad