HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 16, 2021

KIWANDA CHA MAGARI CHA GF VEHICLES ASSEMBLES (GFA) CHACHANGIA DAMU KIBAHA

 


Kiwanda kipya na cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha katika mkoa wa Pwani leo kimeendesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari katika hospitali ya Tumbi mkoani humo.


Tukiwa tunaelekea katika msimu wa sikukuu za mwishoi wa Mwaka kumekuwa na ajali nyingi nchini zimekuwa zikitokea hali iliyopelekea kuzalisha majerui wengi wanaohitaji kuwekewa damu na hivyo benki zetu za damu katika hospitali kuhelemewa.

Kwa kutambua Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kimeamua kuendesha zoezzin la kuchangia damu kwa hiari lililofanywa na wafanyakazi wake katika kiwanda hicho

Akizungumza wakati wa wa zoezi hilo Meneja Mkuu wa Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema wao kama kampuni wamekua na kawaida ya kurejesha kwa jamii kile kidogo wanachokipata na katika hili tumekua tukichangia madawati katika shule na tuliwahiu kupeleka misaada mbali mbali katika vituo vya yatima na hivi leo tumeamua kujitolea Damu mimi na wafanyakazi wenzangu

Kwa upande wa Tumbi akizungumza wakati wa zoeziu hili Afisa ustawi wa Kitengo cha Damu Hospitali hiyo Feliciana Mmasi alisema wao kama tumbi wanamahitaji makubwa ya damu ukizingatia hospitali hiyo inahudumia wagonjwa mbali mbali watokanao na ajali.


Zinazotokea katika mkoa huo kufuatia kuwa kiunganishi cha mikoa mingi ,pia mahitaji kwa mama wajawazito hali inayopelekea matumizi kwa siku ya damu ni kati ya Unit 10-15 hivyo kwa zoezi hili la kuchangia lililofanywa na kiwanda hiki cha magari tumekusanya Unit 15.


Tunashukuru kutokana na uhamasishaji kuwa mdogo na elimu ya uchangiaji damu kutowafikia wananchi wito wangu kwa wananch ni kwamba wajenge tabia ya kuchania damu ili kuokoa wenzetu wenye mahitaji.

Nae Baraka Samsoni mmoja wa wachangiaji damu alisema anajisikia faraja kwa kuchangia damu hii ni mara ya kwanza lakini alikuwa anahofia kama akitoa damu basi anaweza akapata madhara lakini ni tofauti kabisa na nilivyokuwa nadhani.





 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad