Uogozi
 wa Shirika la Childbirth Survival International(CSI) wakiwa kwenye 
picha ya pamoja na walimu wa Chuo cha Urembo Maznat pamoja na washiriki 
waliofika kwenye usaili wa kuwapata vijana wawili uliofanywa chini ya 
CSI na Chuo cha Urembo cha Maznat .
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKA
 la Childbirth Survival International(CSI) tangu kuanzisha kwake miaka 
10 iliyopita limefanya mambo makubwa hasa katika eneo la kupunguza vifo 
vya mama mjazimto na watoto chini ya miaka mitano.
Aliyekuwa
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo 
ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania, Balozi Liberata 
Mulamula(kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwanzilishi wa Shirika la Childbirth Survival International(CSI)Tausi Hamis Kagasheki(kulia) alipokuwa ametembelea banda la Shirika ilo nchini Marekani
Hata
 hivyo kwa mwaka huu wa 2021 limefanya mambo mbalimbali katika jamii ya 
Watanzania na moja ya kazi hizo ni uamuzi wake wa kuwa na programu 
maalum ya kuwasaidia vijana kiuchumi kwa kufanikisha ndoto zao.
Kupitia
 programu hiyo CSI ilijikita katika kuwatafuta vijana wenye ndoto na 
kisha kuzifanikisha.Hivyo ilibeba jukumu, kwanza la kuwatafuta vijana 
wenye ndoto kupitia kongamano maalumu lililofanyika Mombasa jijini Dar 
es Salaam, na baada ya hapo vijana waliopatikana walipatiwa nafasi ya 
kupelekwa Chuo cha Urembo Maznat na kulipia gharama zote, kuanzia ada ya
 masomo hadi nauli za usafiri wa kwenda na kurudi kwa muda wote wa 
masomo.
Madakatari
 kutoka hospitali mbalimbali za Jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi
 ya kuwachunguza watoto Njiti kwa ajili a kujua afya zao ili kuwaepusha 
na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwakabili wakati wa zoezi la kutoa 
huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel 
Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Ukweli
 programu hiyo ya CSI kwa mwaka 2021 imebadilisha maisha ya vijana 
wengi, hata wale ambao hawakubahatika kuchaguliwa, kuanzia hapo 
walibadili mitazamo yao na kuona kumbe wanaweza kutimiza ndoto zao kwa 
kufanya shughuli za kuwapatia kipato.
Hivyo
 wakati mwaka 2021 unakwenda kumalizika, vijana wanabakia na kumbukumbu 
nzuri namna CSI ilivyowashika mkono kwa vitendo, iliona haja ya kuwabeba
 na kufanikisha ndoto zao.
Baadhi
 ya vijana waliobahatika kupata nafasi ya kufadhiliwa masomo na CSI 
wamesema 2021 unabakia kuwa mwaka wa kumbukumbu kubwa katika maisha yao 
itakayochukua miaka mingi kufutika.
Kwa
 kukumbusha tu programu ya kuwasaidia vijana ilianza Januari mwaka 2021 
na katika kongamano la kuwatafuta vijana kwa ajili ya kuwasaidia 
walijitokeza zaidi ya 100 na kati ya hao wawili wakabahatika kupata 
ufadhili wa masomo.
CSI
 imefanya hivyo kwa kuamini vijana ndio wazazi wa kesho , na 
wakiwezeshwa kiuchumi itakuwa rahisi kumudu kuhudumia familia zao, hivyo
 kupunguza changamoto za kimaisha zikiwemo za kumudu gharama za matibabu
 ya afya hasa kupunguza vifo kwa mama mjawazito na mtoto.
David
 Francis ambaye aliibuka mshindi kwenye usaili wa kuwapata vijana wawili
 uliofanywa chini ya CSI na Chuo cha Urembo Maznat akizungumza na 
waandishi wa habari kuhusu namna alivyojiamini mpaka kuwa mshindi kwenye
 shundano hilo.
David
 Francis Matongo ni mmoja ya wanufaika wa mradi wa kusaidia vijana , 
hivyo anasema mwaka 2021 kwake umekuwa wenye bahati kubwa , ndio mwaka 
uliomkutanisha na CSI inayoongozwa na kusimamiwa na wamama wawili wema 
wenye nia ya kusaidia wengine.
"Nikiri
 mwaka 2021 umenikutanisha na CSI, umenikutanisha na watu wema ambao kwa
 kweli wamebadilisha maisha yangu. Ndoto yangu ya muda mrefu ilikuwa ni 
kujifunza urembo , nashukuru CSI wameifanya itimie katika mwaka 
huu,"amesema.
Meneja
 wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival 
International(CSI) Ester Mpanda pamoja na wanafunzi wakipata maelekezo 
kutoka kwa uongozi wa Chuo cha Urembo Maznat mara baaada ya kuwasili 
chuoni hapo kwa ajili ya kuanza masomo ya urembo
Anaeleza
 anakumbuka Januari 2021 CSI walitafuta vijana."Tulikuwa wengi siku ile 
na mimi nikabahatika, Februari 19 nilianza masomo Chuo cha Urembo 
Maznat, tuligharamiwa kila kitu na CSI."
David
 anasema CSI imenisaidia kutimiza ndoto zake na sasa anaweza kumudu 
maisha yake, kupitia ujuzi ambao ameupata amekuwa akifanya shughuli zake
 na kumuingia kipato."Mwaka 2021 kwangu unabakia kuwa mwaka 
mzuri,ahsanteni CSI kwa wema wenu huu."
Wakati
 anazungumza na Michuzi Blog na Michuzi TV katika mwaka huu, David 
ameweka wazi ambavyo sasa anaweza kupamba bibi harusi, kupamba majukwaa,
 kutengeneza kucha, kufanya masaji , kusuka na kufanyia mtu make Up.Yote
 hayo amejifunza kwa ufadhili wa fedha za CSI.
Meneja
 wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival 
International(CSI) Ester Mpanda akizungumza na washiriki wakati wa 
mchakato wa kuwapata vijana hao kupitia usaili uliofanywa chini ya CSI 
na Chuo cha Urembo Maznat ili kuwapata vijana wawili watakaofadhiliwa na
 shitika hilo kwenye masomo ya urembo.
Kwa
 upande wake Meneja Programu za Vijana wa CSI Ester Mpanda wakati 
anazungumza siku walipozindua programu hiyo alieleza wazi CSI wanaamini 
unapomuandaa kijana wa leo katika kutimiza ndoto yake kimaisha, maaa 
yake unamsaidia kiuchumi.
Madakatari
 kutoka hospitali mbalimbali za Jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi
 ya kuwachunguza watoto Njiti kwa ajili a kujua afya zao ili kuwaepusha 
na magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwakabili wakati wa zoezi la kutoa 
huduma za kiafya kwa watoto njiti iliyoandaliwa na Dorris Mollel 
Foundation na kufanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
"Kwa
 muda wote CSI tunaendelea kutimiza majukumu yetu kwa kushirikiana na 
Serikali, kwetu sisi tunajisikia fahari kuona takwimu zinaonesha vifo 
vya mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano vikiendelea 
kupungua.Pamoja na hayo tumeona haja ya kuwasaidia vijana kupitia 
programu hii."
Kuhusu
 CSI, ni shirika la kimataifa ambalo limeanzishwa na wamama wa wawili 
Tausi Hamis Kagasheki anayeishi nchini Marekani ambako ndiko yalipo 
makao makuu ya CSI pamoja na Mama Stella Mpanda anayeishi nchini 
Tanzania.
Wamama
 hao jasiri waliamua kuanzisha shirika hilo ikiwa ni mkakati wa 
kukabiliana au kupunguza vifo kwa mama mjazito na mtoto wakati wa 
kujifungua.Ukweli wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.Kwa kutambua thamani 
ya uhai waliamua kupanua wigo, hivyo CSI , na zaidi wamekuwa 
wakitekeleza majukumu yao katika nchi nyngine .
Meneja
 wa Programu za Vijana kutoka CSI, Ester Mpanda, timu ya Shirika la 
Childbirth Survival International(CSI) pamoja na timu ya Dorris Mollel 
Foundation wakiwafanyia usajili mama na mtoto waliofika kwa ajili ya 
watoto Njiti kufanyiwa uchunguzi na madaktari kutoka hospitali ya 
Muhimbili, Aga Khan na kuandaliwa na Dorris Mollel Foundation 
iliyofanyika Don Bosco jijini Dar es Salaam
Kupitia
 CSI wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kuhusu kutambua afya ya uzazi 
salama kupitia programu mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitoa kwa zaidi 
ya miaka 10 sasa sambamba na kusaidia vifaa vya kujifungulia katika 
hospitali mbalimbali nchini. 
Mbali
 ya Tanzania, CSI ipo pia katika nchi za Somalia, Rwanda, Uganda, 
Marekani, na wanarajia kuwa na tawi nchini Burundi pamoja na Kenya kwa 
nchi za Afrika Mashariki.
Meneja
 wa Programu za Vijana Shirika la Childbirth Survival International(CSI)
 CSI, Ester Mpanda akizungumza kuhusu CSI Tanzania inavyoshirikiana na 
Doris Mollel Foundation wakati wa maadhimisho Siku ya Mtoto Njiti 
Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka 
yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam

No comments:
Post a Comment