Benki ya CRDB yasaini mkataba wa makubaliano na washirika wake kufungua kampuni tanzu DRC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 15, 2021

Benki ya CRDB yasaini mkataba wa makubaliano na washirika wake kufungua kampuni tanzu DRC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakionyesha nakala za makubaliano ya ufunguaji wa kampuni tanzu ya Benki ya CRDB DRC baina ya benki hiyo na mashirika ya IFU la Denmark na NorFund la Norway. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mteule wa Benki ya CRDB nchini DRC, Jessica Nyachiro.
 
=========   =======   ========
 
Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano na washirika wake kibiashara NorFund kutoka Norway na IFU kutoka Denmark kufungua kampuni tanzu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Fleuve De Congo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema katika mkataba huo wa makubaliano taa- sisi hizo zimekubaliana kufanya uwekezaji wa pamoja nchini DRC ambapo Benki ya CRDB itakuwa na uwekezaji wa asilimia 55, huku washirika wake IFU na NorFund wakiwa na asil- imia 22.5 ya uwekezaji kila mmoja.

"Leo ni siku ya furaha sana kwa Benki yetu kwa hatua hii muhimu ambayo tumeifikia katika mchakato wa kupanua huduma zetu hapa DRC. Makabaliano tuliyofikia leo na IFU na NorFund yanatoa mwan- ga mpya katika kufanikisha azma yetu. Baada ya makubaliano haya tunatarajia kukamilisha taratibu zote na kuanza kutoa huduma mnamo mwezi Mei 2021,” amesema Nsekela huku akibainisha kuwa kwa kuanzia Benki hiyo itafungua tawi katika mji wa Lubumbashi.
Rais wa Seneti nchini DRC, Modeste Bahati Lukwebo akizungumza na ujumbe wa Benki ya CRDB wakati ulipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kujenga mahusiano na wadau wa sekta ya fedha nchini humo. Ujumbe wa Benki ya CRDB uliongozwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC, Luteni Jenerali Mstaafu, Paul Metta, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. 
 
“DRC ni mteja wa pili kwa ukubwa wa bandari ya Dar es Salaam, kwa muda mrefu Benki yetu imekuwa ikiwezesha miamala ya biashara kati ya nchi yetu na Congo kupitia mtandao wetu ambao upo kuanzia bandarini hadi mipakani. Sasa tunataka kuboresha na kusogeza huduma zaidi kwa kufungua tawi DRC,” Nsekela alisema.

Alieleza kuwa uhusiano mzuri baina ya Tanzania na DRC unaochagizwa na sera nzuri za na mahusiano mazuri yanayojengwa na Marais wa nchi hizi mbili, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa DRC, Felix Etienne Tshitsekedi, umeushawishi Menejimenti na Bodi ya benki hiyo kuadhimia kuanzisha kampuni tanzu katika taifa hilo kubwa la Afrika ya Kati. “Hatua yetu ya kuanzisha kampuni tanzu nchini DRC inalenga pia kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo nchini humo hususan kwa kuzingatia ujumuishi wa kifedha bado ni mdogo.
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC, Luteni Jenerali Mstaafu, Paul Metta (katikati) akitambulisha ujumbe wa Benki ya CRDB kwa watumishi wa Ofisi ya Rais wa Seneti nchini DRC wakati walipotembelea kwa ajili ya utambulisho na kujenga mahusiano. Ujumbe wa Benki ya CRDB ulion- gozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa kwanza kulia).

Kuna wajasiriamali wengi sana hapa DRC ambao wen- gi pia wanafanya biasha- ra na Tanzania hivyo ni matumaini yangu tutaweza kuwafikia na kujibu changamoto zao,” Nsekela alibainisha na kusema kuwa mkakati wa upanuzi wa Benki ya CRDB utaendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kukuza biashara ya kikanda. “Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza biashara na uwekezaji wa kikanda ambao kama benki ya ndani inayomilikiwa kwa sehemu na Watanzania inaona wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo ili kuharakisha ukuaji wa uchumi wetu,” alisema.

Kwa upande wake, Maka- mu wa Rais wa NorFund, Espen Froyn alisema shirika lake linajivunia kushirikiana na Benki ya CRDB katika kufungua kampuni hiyo tanzu nchini DRC. Froyn alisema anaamini kuwepo kwa Benki ya CRDB nchini Burundi kutasaidia kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini humo na kuboresha maisha wananchi. “Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu na Benki ya CRDB katika miradi mbalimbali nchini Tanzania ambayo imekuwa na manufaa makubwa katika kuongeza ujumuishi wa kifedha. Naamini hata hapa DRC tutaweza kufikia lengo la kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi walio wengi,” amesema Froyn.

Mapema mwaka huu 2021, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitoa kibali kwa benki hiyo kufungua kampuni tanzu nchini DRC. Uidhinishaji wa Benki Kuu ulikamilisha azma ya takriban muongo mmoja ya benki hiyo kupanua wigo wake katika soko la pili la kigeni. Kampuni tanzu ya kwanza ya benki ilifunguliwa nchini Burundi karibu muongo mmoja uliopita na kampuni tanzu ilichukua miaka miwili kutolipa kodi.
Rais wa Seneti nchini DRC, Modeste Bahati Lukwebo (wa pili kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto) wakati ujumbe wa benki hiyo ulipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kujenga mahusiano na wadau wa sekta ya fedha nchini humo. Wengine ni, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC, Luteni Jenerali Mstaafu, Paul Metta (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (watatu kulia) na Mkurugenzi Mtendaji Mteule wa Benki ya CRDB DRC SA, Jessica Nyachiro.

Mwenyekiti wa Benki ya CRDB Dk Ally Laay alise- ma bodi yake iliidhinisha mpango wa kuingia DRC miaka mitatu iliyopita ili kufikia lengo lake la kuungansha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kibiashara na kuifanya benki hiyo kuwa benki kubwa zaidi katika ukanda huu. “Matarajio yetu ya kufikia ndoto hii yalipata nguvu mapema mwaka huu pale benki kuu ilipotupa kibali cha kwenda nchini DRC. Mkutano huu wa leo na washirika wetu, IFU na NorFund, unatuletea karibu zaidi kufikia malengo yetu,” Dk. Laay alisema.

Kwa kukamilisha hatua hiyo, Benki ya CRDB inaunga mkono mpango wa Serikali wa kuinua biashara kati ya nchi hizo mbili. Takwimu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) zinaonyesha kuwa DRC inachukua kati ya asilimia 35 hadi 40 ya mizigo inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Deloitte DRC, Yves Madre ambaye pia anawakilisha kampuni za IFU na NorFund katika uwekezaji wa Benki ya CRDB nchini DRC akizungumza wakati wa mkutano wa kusaini mka- taba wa makubaliano uliofanyika katika hoteli ya Fleuve De Congo, Kinshasa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji mteule wa Benki ya CRDB DRC SA, Jessica Nyachiro. 

Tanzania sasa inataka kuongeza kiwango cha mizigo inayopelekwa na kutoka DRC kwa asilimia 58 katika miaka miwili ijayo. TPA inatarajia kuongeza kiasi cha mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam kwenda na kutoka DRC kutoka tani milioni 1.9 zilizorekodiwa mwaka 2020/21 hadi milioni tatu baada ya miaka miwili ijayo.

Hivi karibuni, Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB ilimteua Jessica Nyachiro kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Tanzu ya Benki ya CRDB nchini DRC. Dk Laay alisema Nyachiro ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mikakati ya Biashara cha Benki hiyo, ana sifa na uzoefu mkubwa kuongoza kampuni hiyo. “Kwa uzoefu, ujuzi na rekodi ya Nyachiro, Benki ya CRDB nchini DRC, itakuwa katika mikono mizuri. Nina hakika kwamba atatusaidia kufikia azma yetu ya kuwa Benki inayoongoza nchini DRC, na kutimiza ndoto za wateja na wadau wetu katika anuwai zote za jamii huku tukisaidia kukuza na kuboresha uchumi.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi Naibu Mkurugenzi wa City Bank DRC, Michael Kayembe (wa pili kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kujenga uhusiano na wadau wa sekta ya fedha nchini humo. Wengine pichani ni, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC, Luteni Jenerali Mstaafu, Paul Metta (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Mteule wa Benki ya CRDB DRC SA, Jessica Nyachiro (wa kwanza kulia).
Rais wa Seneti nchini DRC, Modeste Bahati Lukwebo (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Benki ya CRDB wakati ulipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya kujenga uhusiano na wadau wa sekta ya fedha nchini humo. Ujumbe wa Benki ya CRDB uliongozwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini DRC, Luteni Jenerali Mstaafu, Paul Metta (wa nne kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa nne kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa tano kulia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad