Na Mwandishi wetu, Babati
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Manyara, RAS Caroline Mthapula, amesema
wameshafikisha taarifa ya ahadi zote za ujenzi wa barabara zilizotolewa
na wagombea urais kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.
Mthapula ameyasema hayo kwenye kikao cha bodi ya barabara cha mkoa huo (RCC) kilichofanyika mjini Babati.
Amesema
ahadi zote za miradi yote ya ujenzi wa barabara za lami zilizoahidiwa
na wagombea urais wameshawasilisha Serikalini kwa ajili ya utekelezaji
wake.
"Niwatoe
hofu viongozi na wananchi juu ya barabara zote zilizoahidiwa kujengwa
wakati wa kampeni za uchaguzi kwani sisi kama mkoa tumeshawasilisha
zote," amesema.
Meneja
wa wakala wa barabara nchini (TANROADS) Mkoani Manyara, Mhandisi
Bashiri Rwesingisa amesema ilani ya uchaguzi mkuu wa CCM 2020 inatambua
miradi nane wanayoihudumia.
Mhandisi
Rwesingisa amesema miradi hiyo imegawanyika kwenye makundi mawili ya
ujenzi mpya wa kiwango cha lami na ukamilisha au kuanza upembuzi
yakinifu.
Amesema miradi miwili ambayo usanifu wake umekamilika ni barabara ya Arusha - Kibaya - Kongwa ya urefu wa kilomita 430.
"Serikali
imetenga sh300 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2021/22 kwa barabara ya
Orkesumet - Mirerani kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina,"
amesema.
Awali,
Mbunge wa Jimbo la Hanang' Mhandisi Samweli Hhayuma amesema hayati John
Magufuli na Rais Samia Suluhu walitoa ahadi ya ujenzi wa kilomita 10 za
lami Katesh na barabara ya lami ya Mogitu - Haydom.
Mbunge
wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amesema TANROADS na TARURA
wanapaswa kuandaa bajeti zao mapema ili kuwasilishwa kwa wakati.
Mbunge
wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay amesema ahadi ya ujenzi wa
barabara ya kilomita 190 Karatu - Mbulu - Haydom - Singida na kilomita
10 za lami Dongobesh na Haydom hazijatekelezwa zote.
Mbunge
wa Jimbo la Mbulu Mjini, Paul Zacharia Isaay amesema ujenzi wa
barabara ya Karatu - Mbulu- Singida utarahisha usafirishaji kwa wananchi
wa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment