HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 15, 2021

WIZARA YA AFYA, NIMR KUANZA JARIBIO LA TIBA DAWA ZILIZOFNYIWA UTAFITI

Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), profesa Yunus Mgaya akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo   Novemba 15, 2015 wakati wa akitoa matokeo ya awali ya uchunguzi wa dawa za tiba asilinzinazotumika na watu wenye maambukizi ya Uviko-19 nchini.

Daktari akifafanua takwimu zilizofanyika katika uchunguzi wa dawa za tiba asili zinazotumika na watu wenye maambukizi ya Uviko-19 nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), profesa Yunus Mgaya akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo   Novemba 15, 2015.



KATIKA mwendelezo wa tafiti katika eneo la tiba asili Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kupitia Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR) hivi karibuni kuanza jaribio la tiba 'Clinical Trial' kwa kutumia dawa zilizofanyiwa utafiti wa uangalizi.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya kwa niaba ya Katibu Mkuu Afya, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akitoa matokeo ya awali ya uchunguzi wa dawa asili za tiba asili zinazotumika  na watu wenye maambukizi ya Uviko 19 nchini. 

Amesema kuwa Wazara ya Afya, kupitia Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ikishirikiana na  NIMR imefanya majaribio ya kitafiti ya dawa saba zilizopitishwa na Baraza hilo ili kuhakiki usalama na ufanisi wa dawa hizo za tiba asili.

Dawa zilizofanyiwa utafiti na taasisi mbalimbali ni NIMR  CAF, Covidol, Bingwa, Covatanxa, Planel, Bupifi, (Bupiji), Uzima Herbal Drug. 

Profesa Mgaya amesema kuwa utafiti huo unategemewa kutoa ushahidi kuhusu manufaa ya tiba asili, aidha amesema kuwa Majaribio ya utafiti huo utatoa ushahidi kuhusu matumizi sahihi ya dawa za tiba asili na kuwezesha kuboresha miongozo ya nchi inayohusiana na dawa za tiba asili na tiba mbadala.

Prof. Mgaya amesema Wizara imeshapokea matokeo ya awali ya utafiti huu ulianza mwezi Februari 2021 ambapo matokeo ya awali yanaonesha kuwa dawa hizi tiba asili ni salama, kwa kupitia vipimo vya maabara vilivyokuwa vinafanyika vya figo, Ini kwenye damu, hakuna athari zilizoonekana kwa wagonjwa wa UVICO-19 waliokuwa wanatumia dawa hizi.

Amesema NIMR imewashirikisha watafiti wakubwa kutoka taasisi mbalimbali, ambapo ni wafanyakazi wa afya kutoka hospitali zilizoshiriki utafiti huo, chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishii Muhimbili(MUHAS), chuo kikuu cha Sokoine, (SUA) na chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Prof. Mgaya amewasihi wananchi kutumia dawa za tiba asili na tiba mbadala ambazo zimesajiliwa na baraza la tiba asili na tiba mbadala kwa huwa hizi ndio zilizothibitishwa kuwa na usalama unaokubalika.

Wizara ya afya inawakumbusha wananchi kuendelea kutumia afua zote kama zinavyoelekezwa ikiwemo kuchanja, kuvaa barakoa na kunawa mikono na sabuni na majitiririka katika kujikinga na maambukizi ya Uviko- 19. 

Hivyo wananchi wanashauriwa kwenda kuchanja katika kituo cha chanjo kilichopo karibu kwakuwa chanjo ni afua madhubuti inayoongeza kinga ya mwili ambayo itasaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi yanayoweza kusaaisha vifo vitokanavyo na Uviko-19.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad