Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael amewataka watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na watumishi wote wa umma kwa ujumla, kufuata kanuni, taratibu, sheria pamoja na miongozo ya utumishi wa umma katika utendaji kazi wao wa kila siku ili kuepuka kutokufanya makosa ya kiutumishi.
Dkt. Michael ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Novemba,
2021 alipofanya ziara katika taasisi ya BRELA ikiwa ni sehemu ya
utaratibu wa Wizara yao ya menejimenti ya utumishi wa umma na utawala
bora, kutembelea ofisi na taasisi za Serikali ili kujua changamoto na
matatizo yanayowakabili watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi.
Dkt.
Michael amesema watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata
kanuni, sheria na taratibu ambazo zimewekwa kuepuka makosa ya kiutumishi
Dkt.
Michael ameeleza kuwa Maafisa Utumishi wanawajibu wa kuwa na nyaraka
zote za kiutumishi na kuhakikisha kuwa watumishi wote wanazifahamu
nyaraka hizo kwa kuwa siyo nyaraka za siri, hii itasaidia watumishi
kujua haki, stahiki pamoja na wajibu wao na kuondoa uwezekano wa
watumishi kufanya makosa ya kiutumishi kwa kutokutambua sheria na
miongozo inayowasimamia, lakini pia, aliongeza kusema kuwa hatua hiyo
itasaidia kuondoa malalamiko ya watumishi mahala pa kazi.
“Mtumishi
anapokuwa na malalamiko ya kiutumishi morali ya kufanya kazi hupotea na
hata malengo yaliyotakiwa kufikia na taasisi husika hayafikiwi
kikamilifu, ndio maana sisi viongozi kutoka utumishi tunaona ni bora
tuwe tunawazungukia watumishi ili kuweza kuwafikia kwa ukaribu na
kusikiliza shida zao na kuyatatua mapungufu madogo madogo ambayo tunaona
yanaweza kutekelezwa papo kwa papo tunayafanyia maamuzi,” ameeleza Dkt.
Francis
Pia, watumishi wa BRELA wameelekezwa kuheshimu mamlaka
kwa kufuata maadili na viongozi wanaowasimamia watumishi wa umma
kutotakiwa kunyanyasa watumishi walioko chini yao kwa namna yoyote ile.
Akaongeza kusema kuwa viongozi watambue kila mtumishi anatumia muda
mwingi eneo la kazi na siyo nyumbani, hivyo kila kiongozi anawajibu wa
kujenga mazingira mazuri sehemu zao za kazi ili watumishi waweze
kufurahia kazi.
Dkt. Michael amesema kuwa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko wazi kwa watumishi
wote na itaendelea kutembelea taasisi za umma ili kusikia matatizo yao
kwa lengo la kujenga na kuinua morali ya kazi kwa watumishi wa umma.
Kwa
upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa ameeleza
kufurahishwa kwa ujio wa Naibu Katibu Mkuu kwani imekuwa ni fursa nzuri
ya kukutana na watumishi na watumishi wamepata nafasi ya kueleza
changamoto zao kwa uwazi na kupatiwa ufumbuzi papo kwa papo.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano- BRELA
No comments:
Post a Comment