HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

WANAWAKE WENYE MAMLAKA WAONYWA WASIVIMBIE MADARAKA

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.
Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Ndugai ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma  katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi. Spika amesema Taifa linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama.

"Lakini kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi," amesema  Ndugai.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad