WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI VINARA SHINDANO LA MICHORO YA USALAMA BARABARANI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 4, 2021

WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI VINARA SHINDANO LA MICHORO YA USALAMA BARABARANI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mtopepo B visiwani Zanzibar Khalid Mohamed Said(aliyevaa kofia) akiwa na wanafunzi wenzake wa shule hiyo wakiwa wameshika kikombe cha ushindi wa mchoro wa Usalama Barabarani kwa mwaka 2021 yaliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Amend.Utoaji wa zawadi kwa wanafunzi na shule ambazo zimeibuka washindi kwenye shindano limefanyika leo katika Shule ya Msingi Kiembe Samaki ,Zanzibar ambapo Meya wa Zanzibar alikuwa Mahamoud Mohamed Mussa alikuwa mgeni rasmi.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MEYA wa Jiji la Zanzibar Mahamoud Mohemed Mussa ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi Zanzibar kuchukua hatua kali kwa waendesha magari na vyombo vya moto ambao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwani kumekuwepo na wimbi kubwa la ajali ambazo nyingi zinatokana na uzembe wa baadhi ya watumiaji wa vyombo hivyo.

Akizungumza wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi walioshinda shindano la michoro ya Usalama Barabarani kwa shule za Msingi Zanzibar ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma pamoja na Shirika la Amend Meya Mussa aliyekuwa mgeni rasmi amesema ni muhimu mafunzo hayo yakaendelea kutolewa na katika shule nyingine visiwani humo.

Amesema anaamini malengo yaliyokusudiwa yamefikiwa na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi hao hasa kupunguza ajali huku akilisisitiza umuhimu wa kuhakikisha Jeshi la Polisi Zanzibar kuchukua hatua kali kwani kumeibuka wimbi la watumia vyombo vya moto amba hawafuati sheria za usalama barabarani na wengta leseni.

"Kuna wimbi la waendesha vyombo vya moto ambao hawana leseni na matokeo wamekuwa wakichangia uwepo wa ajali za barabarani, na kwa mazingira ya aina hiyo utaona haja ya uwepo wa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kupunguza ajali za barabarani.Takwimu zinaonesha kumekuwa na idadi kubwa ya watu duniani kote ambao wanapoteza maisha ,hivyo mafunzo hayo ni vema yakaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali,"amesema Meya huyo.

Kwa upande wake, Meneja Mauzo Rejareja wa Puma, Venessy Chilambo amesema lengo la kutoa mafunzo ya usalama barabarani visiwani Zanzibar ni kupunguza ajali za barabarani hasa ikizingatia kuwa Mji huo idadi ya magari imekua ikiongezeka kwa wingi kila siku.

" Mpango huu wa usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi miaka 9 iliyopita ambapo zaidi ya shule 100 zimefikiwa na wanafunzi zaidi ya 120,000 mikoa mbalimbali wamepata mafunzo hayo kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Tukio hili la utoaji zawadi linahitimisha mradi huu kwa kipindi cha mwaka 2020-2021 uliofanywa na kampuni ya Puma kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la AMEND. Mpango huu ulihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani na uchoraji wa picha katika shule 5, ambapo wanafunzi wasiopungua 20,000 walipata mafunzo hayo," Amesema Chilambo.

Chilambo ameendelea kusema kuwa " Puma tunafanya biashara Zanzibar hivyo hii ni njia mojawapo ya kurudisha tunachokipata kupitia mpango huu. Mafunzo haya ya usalama barabarani na uchoraji kwa watoto wa Shule za msingi ni endelevu na lengo ni kuwaelimisha watoto juu ya usalama barabarani ili wawe mabalozi kwa wengine na kwa wao wenyewe hadi watakapokuwa wamekuwa watu wazima,"

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni a Michezo Fatma Hamad Rajab amesema amefarijika kuona wanafunzi wamepata elimu ya usalama barabarani na kwamba elimu hiyo itasaidia kuwafanya wawe wanavuka barabara kwa usalama.

Ameongeza hata walimu ambao ndio walezi wa wanfunzi wawapo shuleni watakuwa na kazi rahisi y kuagalia usalama watoto hao wanapovuka barabara.Pia amewapongeza walimu waliosimamia wanafunzi kuchora michoro ya usalama barabarani kupitia shindano hilo kwani mbali ya kushiriki wamesaidia kuibua vipaji vya wachorajo na hilo ni jambo jema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Salum Amir Ngayan mesema kampeni hiyo ambayo ni ya aina yake imekuwa maalum kwa ajili ya kuzuia ajali visiwani Zanzibar kwani kumekuwa na changamoto ya ajali.

Amesema ajali za barabarani zimekuwa zikisababisha vifo vya Watanzania wakiwemo vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa na kwamba ajali nyingi zinatokana na kutoheshimu sheria za usalama barabarani zikiwemo alama."Kuna madereva hawatii alama za barabarani hivyo watoto wakiwa na uelewa wa jinsi ya kuvuka tutakuwa tumepunguzza ajali ambazo si za lazima.

Wakati Meneja wa Programu wa Shirika la NVCT ambalo limeshiriki katika kutoa mafunzo ya usalama Barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi Zanzibar Ali Hemed Ali amesema jumla ya shule tano zimepata mafunzo hayo na hadi sasa zaidi ya wanafunzi 40,000 Zanzibar wamefikiwa.

Mashindano yamefikia kilele chake leo Visiwani Zanzibar kwa wanafunzi walioshinda kupata zawadi zao ambapo mshindi wa kwanza amepata Sh.500,000 wakati shule yake itapata Sh.milioni nne

Kwa upande wa Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Amend amesema Neema Swai amesema mradi huo mradi ambao umekuwa endelevu na kwa Zanzibar hii ni mara ya pili huku akifafanua kwamba takwimu zinaonesha watu milioni 1.35 wanakufa na wengine zaidi ya milioni 50 wanajeruhiwa na wengi wao ni watoto na watu wenye umri chini ya miaka 25.

"Tunawashukuru NVCT kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa katika kufanikisha utolewaji wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani Zanzibt na tunatambua muhimu wa kuwaanda watu wakiwa wadogo kwani hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa kuheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani.Hivyo tuko Zanzibar kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu hiyo kwa lengo la kupunguza ajali,"amesema.

Katika mashindano hayo Shule ya Msingi Mtopepo B imeibuka mshindi wa jumla kwa kupata Sh.milioni nne wakati mwanafunzi wake anayesoma darasa la sita Khalid Mohamed Said ameibuka mshindi na kuzawadiwa Sh.500,000.

Meya wa Jiji la Zanzibar Mohamoud Mohamed Mussa(watatu kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa Shindano la mchoro wa Usalama Barabarani kwa Shule za Msingi Zanzibar ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Amend Khalid Mohamed Said anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Mtopepo B visiwani Zanzibar.Wengine katika picha hiyo ni viongozi kutoka kampuni ya Puma, Amend na walimu.Utoaji zawadi kwa washindi wa shindano hilo umefanyika Shule ya Msingi Kiembe Samaki.


Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mtopepo Visiwani Zanzibar Khalid Mohamed Said akiwa ameshika kikombe cha ushindi baada ya kuibuka mshindi wa shindano la mchoro wa usalama Barabarani kwa mwaka 2021.Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Aamend.
Meya wa Jiji la Zanzibar Mahamoud Mohamed Mussa(wa nne kulia) akiwa na viongozi wengine na wawakilishi kutoka Kampuni ya Puma na Amend wakiangalia mchoro wa shindano la usalama barabarani visiwani Zanzibar ambapo shule tano zimeshiriki.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la Usalama Barabarani mwaka 2021 lililoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa ushirikiano na shirika la Amend .Utoaji zawadi umefanyika Shule ya Msingi Kiembe Samaki, shule tano visiwani Zanzibar vilishiriki shindano hilo na Shule ya Msingi Mtopepo B imeibuka mshindi wa jumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad