TTCL PESA YAZINDUA T-PESA APP LEO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 2, 2021

TTCL PESA YAZINDUA T-PESA APP LEO

kurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) namna ya kutumia 'T-PESA APP' leo jijini Dar es Salaam wakati alipozinduwa huduma hiyo. Kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja T-Pesa, Dorothy Urio pamoja.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) alipokuwa akizinduwa huduma ya 'T-PESA APP' leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja T-Pesa, Dorothy Urio pamoja na Afisa Mauzo, Emerco Mashelle wakifuatilia.

Sehemu ya wafanyakazi na maofisa wa T- Pesa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya 'T-PESA APP' leo jijini Dar es Salaam.

Na Joachim Mushi
KAMPUNI ya TTCL PESA imezinduwa huduma ya T-PESA APP ambayo itawarahisishia wateja wa mtandao huo kupata huduma mbalimbali za malipo kwa kutumia mtandao huo.

Akizinduwa huduma hiyo, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde alisema huduma hiyo ni miongoni mwa maboreshomakubwa wanayoyafanya ili kuwarahisishia wateja wao kufanya huduma mbalimbali kwa haraka zaidi.

“Kampuni ya T-PESA imeendelea kujikita kidigitali zaidi kwa kuzindua leo huduma ya T-PESA APP. Huu ni mfumo rahisi wenye ufanisi kwa wateja wanaotumia huduma za T-PESA," aliwaeleza waandishi wa habari Mkurugenzi huyo wa T-PESA.

Akifafanua zaidi alisema kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kufanya malipo mbalimbali popote walipo na kwa haraka zaidi, ikiwemo kulipia bili za maji, umeme, ving’amuzi na faini mbalimbali za Serikali.

Aidha aliongeza kuwa huduma hiyo inaenda kuwarahisishia kazi mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwani sasa kwa kutumia T-PESA APP wataweza kulipia viingiio vya mechi mbalimbali za mpira kwa NCARD.

"Huduma ya QR Code ni njia ya haraka na rahisi ya kufanya malipo ambayo kwa T-PESA APP inawezekana katika maduka, migahawa na maeneo mbali mbali nchini ikiwemo vituo vya petrol vya Puma. Wateja pia wanaweza kuangalia salio bure, kununua au kutuma muda wa maongezi," aliongeza.

Hata hivyo, aliwaomba Watanzania na Wateja kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za T-Pesa na kama bado hawana laini za TTCL basi wajisajili mara moja ili kufurahia huduma kwa bei nafuu.

"Huduma hii ya T-PESA APP inapatikana kwenye ANDROID kwa kupakua kupitia google playstore. Tunajivunia huduma hii kwani T-PESA APP ni tofauti na APP nyingine za mitandao ya simu kwa sababu ina huduma ya kipekee ya kumuwezesha mteja wetu kununua tiketi za mpira wa miguu kwenye mechi zote zinazochezwa Tanzania Bara," aliongeza Bi. Mkudde.

Amesema Kampuni ya T-PESA itaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta mbalimbali ili kuondoa changamoto zilizopo na kuendana na matumizi ya mifumo ya kidigitali na kupelekea upatikanaji wa huduma zake kwa wakati na urahisi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad