Afisa Msimamizi Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Jackline Lutare (kulia) akisikiliza changamoto mbalimbali za Mlipakodi wa eneo la Majimoto mkoani Katavi wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Morgan Isdor (kushoto) akimuelekeza Mlipakodi wa eneo la Majimoto mkoani Katavi kuhusu namna ya kuperuzi tovuti ya TRA na kupata huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao kupitia simu janja yake, wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.
Afisa Msimamizi Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Mercy Macha (kulia) akisikiliza malalamiko ya Mlipakodi wa eneo la Majimoto mkoani Katavi kuhusu makadirio ya kodi katika biashara yake wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi ya mlango kwa mlango inayoendelea mkoani hapo.

No comments:
Post a Comment