HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 17, 2021

SERIKALI YAKEMEA URASIMU DHIDI MAAFISA MAWASILIANO WA TAASISI

 

Waziri wa Elimu  Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa Taasisi za elimu Nchini kuwapa  mamlaka maafisa Habari wa taasisi hizo kufanya majukumu yao  ikiwa na lengo la kuzisemea vyema taasisi na serikali katika kutolea ufafanuzi wa taarifa mbalimbali kwa jamii ili wananchi waweze kufahamu namna Serikali ilivyowekeza fedha nyingi  katika kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu nchini.

 

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichowashirikisha Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ambapo amesema mafanikio  makubwa katika sekta ya elimu si ya kificho, hivyo ni vyema yakawa yakitolewa kwa wananchi ili waweze kufahamu ni namna gani Serikali yao ilivyowekeza katika kuhakikisha Watanzania wanapata elimu bora.

 Amesema ameshuhudia mara nyingi Maafisa Mawasiliano hao wamekuwa wakijielekeza zaidi katika kutangaza matukio ya viongozi wanapokuwa na shughuli mbalimbali katika taasisi zao na baada ya matukio hayo hakuna kinachoendelea. Amewataka Maafisa hao kubadili utaratibu huo na kujikita zaidi katika kutangaza mafanikio makubwa ya uboreshwaji wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

 

 “Nimefurahi kwamba katika mafunzo haya wakuu wa Taasisi wameshiriki, naamini ushiriki wenu utaleta mabadiliko na kuwa wepesi wa kutoa habari fasaha na kwa wakati.  Tuepuke urasimu, yapo mambo yanatokea kwenye vyombo vya habari na mitandao lakini mmekuwa wazito kutoa mrejesho kwa wananchi, ni vizuri kufanyia kazi ili kuepuka mkanganyiko,” amesema Waziri Ndalichako

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad