HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

RAIS SAMIA APONGEZWA NA BAKWATA MWANZA UENDESHAJI WA NCHI

 

NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, limempongeza,Rais Samia Suluhu Hassan,kwa namna anavyoendesha nchi,kusimama na wananchi wake kuhakikisha wanapata maendeleo na wananufaika kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Pia limeipongeza serikali mkoani humu kwa kuendesha zoezi la kuwapanga na kuwahamisha wafanyabiashara wadogo (Machinga) kwa amani bila vurugu kutoka kwenye maeneo hatarishi na yasiyo rasmi, kwenda kwenye maeneo ya rasmi ya kufanyia biashara.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kebeke,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu suala la machinga,chanjo ya Uviko-19 n miradi ya maendeleo ya waislamu.

“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais Samia kwa kusimamia na kuendesha nchi kwa kipindi kifupi cha takribani miezi saba kafanya mengi ya maendeleo,ameonyesha yuko tayari kusimama na wananchi wake.”

Alisema kiongozi mkuu huyo wa nchi aliwaelekeza wasaidizi wake kuwapanga upya machinga na kuwapangia maeneo ya biashara ili waondoke pembezoni mwa barabara wawatendee haki kwa utu badala ya kuwafukuza.

“Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel,kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya ya wakurugenzi halmashauri kutoa elimu kwanza kwa machinga,kuandaa maeneo ya kuwapeleka na kuchukua orodha yao,kwa hilo wanastahili pongezi kubwa,jiji limetulia na mji uko safi na salama,”alisema Sheikhe Kabeke.

Alifafanua kuwa kukamilika kwa zoezi hilo Mkoa na Jiji la Mwanza sasa linarudi kwenye ubora na heshima yake ya usafi kwa miaka 6 ambapo kabla ilikuwa haifahamiki mji uko wapi,biashara zilifanyika holela hadi barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi na watumiaji wengine.

Kiongozi huyo wa kiroho alisema hali ilikuwa mbaya na laiti ingetokea ajali watu wengi wangepoteza maisha, hivyo elimu iliyotolewa iliwaingia machinga wakapima maji na unga wakaridhia kuondoka ni jambo la kuwapongeza wafanyabiashara hao.

Sheikhe Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kmati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza, aliipongeza serikali na kuwataka wananchi na wafanyabiashara wadogo kuzoea utaratibu unaowekwa na serikali badala ya kujifanyia biashara holela na mahali popote.

Aidha limeshauri wanahabari kutafuta habari kwenye vyanzo vya kuaminika ili kuepuka kuandika habari zenye kuvunja amani,kuchochea migogoro na kuzua taharuki kwenye jamii kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

“Baadhi ya wanahabari hawatendi haki ukizingatia suala hili ni kwa maslahi ya umma na si la mtu mmoja, niwashauri wapate habari kutoka kwa vyanzo sahihi,hivi eneo la Makoroboi ni kubwa kuliko Mchafukoga! Makoroboi ni uchochoroni huwezi kupalinganisha na Mchafukoga,twendeni tulikopangiwa tufanye biashara,” alisistiza Sheikhe Kabeke.

Kuhusu suala la chanjo ya Uviko-19,alisema Mhadisi Gabriela akishirikiana na Mganga Mkuu wa Mkoa,Dk. Thomas Rutachunzibwa na wataalamu wa afya,wakiwemo maaskofu na masheikhe walishiriki kutoa elimu kwa jamii kuhusu chanjo ya JJ.

“Kila jambo lina kwenda na kiongozi, RC amejipambanua sana kwenye masuala ya msingi,amesimamia chanjo vizuri,machinga na sasa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwakani, tujitokeze kuhesabiwa kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi,”alishauri.

Aidha Sheikhe Kabeke alisema BAKWATA imeanza kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kujenga vituo vya afya kila wilaya ili kuunga mkono juhudi za serikali kwenye sekta hiyo kwa maslahi ya waislamu,jamii na Watanzania bila kujali itikadi zao za kiimani na kisiasa.

“Novemba 14, saa 2 asubuhi tutakweda Kata ya Kiseke kuchimba msingi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Wilaya ya Ilemela,kituo ambacho kitato huduma kwa jamii ya watu wa dini zote naamaini safari hiyo ya Ilemela itakamilika kwa maslahi ya Watanzania, waislamu na jamii yote bila kujali itikadi zao,” alisema na kuongeza ujenzi huo pia utafanyika Misungwi, Sengerema, Ukerewe, Magu, Kwimba na Nyamagana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad