Nchi za Afrika zatakiwa kuchangia mafanikio ya 'African court' - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 1, 2021

Nchi za Afrika zatakiwa kuchangia mafanikio ya 'African court'

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza mara baada kufunguliwa kwa Mkutano wa Utekelezaji na Athari za Maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu. Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Novemba Mosi, 2021.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Utekelezaji na Athari za Maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu. Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Novemba Mosi, 2021.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, Imani Aboud akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Utekelezaji na Athari za Maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu. Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Novemba Mosi, 2021.

Baadhi ya wadau wa Mahakama wakisikiliza mada katika Mkutano wa Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na watu uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Novemba Mosi, 2021.

NCHI za Afrika kwa pamoja zimetakiwa kuchangia katika mafanikio ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa kutekeleza ipasavyo maamuzi yanayotolewa na taasisi hiyo ili kuweza kuendelea kutoa haki kwa wananchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo leo Novemba Mosi, 2021 jijini Dar es Salaam katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Utekelezaji na Athari za Maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, iliyosomwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman.

Amesema hatua hiyo itawahakikishia walalamikaji wanaofika mbele ya Mahakama hiyo kula matunda ya kesi zao na pia itaonyesha dunia nzima kwamba nchi za Afrika sasa zinachukulia kwa uzito, ulinzi na uendelezaji wa haki za binadamu.

"Japo kuwa kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali katika ufanyaji kazi wa mahakama hii lakini pia tangu kuanzishwa kwa kwake mwaka 1998 mahakama hii imekuwa na mafanikio mengi katika kulinda haki za binadamu na watu." Amesema Mwinyi

Amesema, ni nchi 31 tu ndio zimejiunga na umoja huo na kwamba bado kuna matatizo kwani kuna tamko limetolewa la kwamba Taasisi na watu binafsi waweze kupeleka malalamiko yao moja kwa moja kwenye mahakama hiyo ingawa bado hazijakubaliana.

Kupitia mkutano huu, changamoto zilizopo zitatuliwa kwani lengo ni kutafuta kasoro zilizopo ili tuweze kuzitatua na kutafuta njia gani tufanye ili watu wote waweze kupata haki zao pamoja na Taasisi mbalimbali na nchi pia.

Aidha imebainishwa katika ripoti ya shughuli za Mahakama ya mwaka kwa Umoja wa Afrika (AU) kwamba utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama hiyo katika nchi wanachama uko chini sana na takwimu zinaonesha ni asilimia saba tu ya nchi hizo ndio zinatekeleza maamuzi, takwimu ambazo ni chache ambazo mahakama haipaswi kujivunia.

Mkutano huu wa siku tatu unafanyika katika muda muafaka na kwamba washiriki watajadili na kuibua hoja nzito za namna bora ya kumaliza changamto mbalimbali zinazoikabili Mahakama hiyo ya Afrika hususani suala la utekelezwaji wa maamuzi yake kwani ni Taasisi waliyoianzisha wenyewe na ni jukumu la waafrika kuhakikisha hawashindwi kufikia malengo yao.

Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Imani Aboud amesema baada ya mkutano huo, wanategemea Kukubaliana njia bora zaidi za kuboresha kazi na majukumu ya mahakama hiyo sababu, watu watapokutana na kuzungumza basi ni rahisi kufikia muafaka kwenye masuala ambayo yamekuwa ni changamoto.

Mnapokutana na kuzungumza mnapata muafaka wa pamoja katika masuala ambayo yanaleta changamoto na changamoto kubwa tuliyonayo ni utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama ya Afrika ndio maana tumewaita wadau wote muhimu ili tuzungumze ni changamoto gani ambazo wao wanaziona zinawakwamisha katika kutelekeza maamuzi ya Mahakama.” Amesema bi. Imani

Amesema wakati Mahakama hiyo ikisherehekea miaka 15 tangu kuanzishwa kwake kati ya maamuzi kumi yaliyotolewa ni uamuzi mmoja tu ndio unatekelezwa na nchi wanachama, nchi chini ya sita waanzilishi wa Mahakama hiyo zinatambua mamlaka ya Mahakama hiyo na ni nchi 31 pekee ndio zinatambua shughuli za Mahakama hiyo na taswira ambayo si nzuri, haionyeshi heshima kwa Umoja wa Afrika wala kwa Mahakama hii ya Afrika na Wananchi wa Afrika.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar sa Salaam, amesema anaamini mazungumzo katika mkutano huo yatatatua changamoto ndogo ndogo zinazotokea katika mahakama hiyo ya Afrika kwa sababu mahakama hiyo ni ya waafrika na waafrika wenyewe ambao wanafahamu mustakabali wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad