HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 2, 2021

NAMTUMBO YAONGOZA UTOAJI CHANJO MKOA WA RUVUMA

 

NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Namtumbo yaongoza utoaji  wa chanjo Mkoani Ruvuma, akisoma taarifa ya chanjo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu alisema wilaya ya Namtumbo inaongoza katika mkoa wa Ruvuma katika kuchanja wananchi wake chanjo ya Uviko 19 aina ya Sinopharm.

Dkt Ningu alisema hayo katika ziara ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma wilayani Namtumbo katika kata ya Luchili kuzungumza na wananchi wa kata ya Luchili kutatua mgogoro wa makao makuu ya kata ambao wananchi wa kata hiyo wanagombania.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Lucia Kafumu alisema sababu kubwa ya kuchanja wananchi wengi wilaya ya Namtumbo ilikuwa ni uelewa walioupata kuhusu elimu waliyoipata kutoka kwa watalaamu wa afya , viongozi wa serikali, dini ,chama na kwa kushirikiana na wananchi wengine katika vijiji mbalimbali wilayani humo walioweza kusaidia kutoa elimu kwa wananchi wenzao.

Kafumu alidai wakati timu ya wataalamu wa afya inapita kutoa elimu katika vijiji kwa njia ya mikutano ya Hadhara ilipata ushirikiano wa viongozi wa serikali,viongozi wa dini,chama na baadhi ya wananchi ambao walijitokeza kuelimisha wananchi wenzao .

Aidha kafumu alisema kitendo cha viongozi wa serikali kutoka katika vijiji vya wilaya ya Namtumbo kujitokeza kuchanja ndicho kilichosaidia hata wananchi wengi wajitokeze katika kupata chanjo baada ya kuona viongozi wao kuchanja na hata sasa wananchi wanajitokeza kwa wingi katika zahanati zao kuchanja.

Mratibu wa chanjo katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Elias Patrick Boniface alisema wilaya ya Namtumbo ilipokea chanjo dozi 5300 ya UVIKO 19 aina ya Sinopharm tarehe 27 mwezi oktoba mwaka huu na kuzisambaza katika vituo vya kutolea huduma za afya nakufikia tarehe 31 mwezi oktoba mwaka huu dozi hizo ziliisha na kufikia asilimia 100 katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambapo mpaka leo tarehe 2 Novemba vituo vya kutolea huduma zimeishiwa dozi za chanjo hizo na Halmashauri imeomba dozi zingine 500 kutoka ofisi ya mratibu wa Chanjo Mkoa wa Ruvuma .

Mratibu wa chanjo mkoa wa Ruvuma Wilbroad Mvile alikiri kupokea maombi ya kuomba dozi 500 za chanjo ya UVIKO 19 ya Sinopharm na kusema kuwa tayari dozi hizo zilizoombwa zimetolewa kwa wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kwenda kugawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ili zoezi la uchanjaji lisisimame alisema Mratibu Huyo.
Mpaka leo tarehe 2 mwezi Novemba 2021Halmashauri imemaliza dozi 5300 na kupokea dozi zingine500 hali iliyoifanya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuwa ya kwanza katika uchanjali katika mkoa wa Ruvuma.

Tathimini ya uchanjaji mkoa wa Ruvuma wilaya ya Namtumbo ni ya kwanza kwa kuchanja,ikifuatiwa na Halmashauri ya mbinga na yatatu ni halmashauri ya Tunduru huku Halmashauri ya Nyasa ikiwa nafasi ya Nne

Zingine ni Halmashauri y Songea Manispaa Ambayo imeshika nafasi ya 5,na Halmashauri ya Madaba imeshika nafasi ya 6 huku Halmashauri ya mbinga mji ikishika nafasi ya 7 na Halmashauri ya Songea ikishika nafasi 8 kimkoa katika uchanjaji.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 54 zinazohusika na utoaji wa huduma za chanjo ya Uviko19 ya Sinopharm ambavyo wananchi wanavitumia katika kupata chanjo hiyo na kusababisha wilaya kuongoza katika mkoa katika zoezi la uchanjaji.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad