Na Mwandishi wetu, Hanang'
TIMU
ya soka la wanawake ya daraja la kwanza ya Mount Hanang' Queens ya
Wilayani Hanang' Mkoani Manyara, imeibugiza mabao 2-0 timu ya Gitting
Veterans.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Gitting juzi mabao ya timu hiyo yalipatikana kwenye kila kipindi.
Mshambuliaji
wa timu hiyo Agnes Chuwa alifunga bao la kwanza dakika ya 17 kwa kichwa
baada ya kona iliyopigwa na kiungo mshambuliaji Fatuma Yassin.
Kiungo
mkabaji Rachel Samwel ameipatia bao la pili timu hiyo kwenye dakika ya
55 ya mchezo huo, baada kumalizia shuti kali la kiungo mshambuliaji
Fatuma Yassin.
Mdhamini
wa timu hiyo Paul Phares Mnyandwa amesema ataipeleka timu hiyo wilayani
Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki.
Mwenyekiti wa timu hiyo mwalimu Gisella Msofe amesema timu hiyo ya daraja
la kwanza inaendelea na mapambano hadi ipande ligi kuu.
la kwanza inaendelea na mapambano hadi ipande ligi kuu.
Kocha
mkuu wa timu hiyo, Robert Massay amesema Mount Hanang' Queens ina uwezo
mkubwa na inaweza wa kushinda timu kubwa za Simba Queens na Fountain.
This written piece gives fastidious understanding yet.social media
ReplyDelete