HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 7, 2021

KAMPUNI YA HEBO YAPUNGUZA GHARAMA ZA MAFUNZO YA USIMAMIZI MIRADI

Mkurugenzi wa Ushauri wa Kampuni ya Hebo, Martin Hekeno akizungumza na waandishi wa habari jijini wakati wa kusheherekea siku ya kimataifa ya usimamizi miradi ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Novemba 5.


KAMPUNI ya Usimamizi wa Miradi ya HEBO imesheherekea siku ya kimataifa ya usimamizi wa Miradi ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Novemba 5 kwa kutambua mchango wa wasimamizi wa katika uchumi wa dunia na Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ushauri wa Kampuni ya Hebo, Martin Hekeno amesema kitu wanachojivunia ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi na waliomaliza chuo na wamepunguza gharama za utoaji mafunzo

"Leo hii kwasababu ni siku ya usimamizi miradi duniani tumeamua kutoa ofa kubwa kwa kupunguza gharama ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi na waliomaliza chuo hivi karibuni kwa asilimia 70 kuanzia leo Novemba 5 mpaka Desemba 2021." Amesema Hekeno

Hekeno amesema kuwa katika maadhimisho ya mwaka huu 2021 wamejikita zaidi katika utoaji mafunzo kwenye sekta ya Nishati kwani kunamiradi mikubwa ya gesi na mafuta na inaendelea hapa nchini.

"Tunaamini kwamba usimamizi wa miradi unapokuwa vizuri hata uchumi wetu unakua, tunatengeneza wataalamu na wazalendo wa kusimamia miradi yetu ili Tanzania iweze kukua kiuchumi." Amesema Hekeno

Akizungumzia uendelezaji wa miradi hapa nchini hekeno amesema wanaongeza uelewa kwa wanaokidhi vigezo vya Usimamizi wa miradi ili waweze kusimamia inavyotakiwa.

Amesema kuwa ili kuhakikisha miradi hapa nchini inafanikiwa Hebo wameungana na kampuni ya kimataifa ya usimamizi wa Miradi ya Project Management Institute (PMI) ili kutoa mafunzo yenye viwango vya kimataifa na kuleta hapa nchini haina haja ya kutafuta wataalamu wa miradi kutoka nje ya nchi.

Ametoa wito kwa wasimamizi wa miradi kujiandikisha na kujifunza jinsi ya kusimamia miradi.

Mdau wa Usimamizi wa Miradi, Keneth Mtaonga anesema kuwa ujuzi unahitajika katika kufanya miradi ya Nishati nchini ili kuendeleza kwa manufaa ya maendeleo ya nchi.

Ametoa mfano mradi ya Upepo kwa kupanga unawezaje kuchukua vifaa vilivyopo Bandarini na kupeleka Singida kutengeneza nishati ya upepo.

Amesema kuwa kunamwingiliano mkubwa wa fani kati ya Meneja mradi na miradi iliyopo hapa nchini.

Kwa upande wake mwanzilishi na Mkurugenzi wa mafunzo wa kampuni ya Hebo Consult Bulla Hekono amesema kuwa, katika kusherekea siku ya uendelezaji wa miradi duniani (Project Management day) wamejumuika na watendaji wa miradi na kufanya mijadala mbalimbali kuhusiana na miradi mbalimbali inayoendelea nchini hususani katika sekta ya nishati mbadala.

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali ya ufanisi katika kuendeleza sekta hiyo hususani kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya uendelezaji wa miradi ili kuwapa ujuzi na ufanisi zaidi na hiyo ni kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya uendelezaji wa miradi duniani ili waweze kutambulika kimataifa na kuendeleza miradi inayoendelea nchini kwa ufanisi, gharama nafuu na viwango bora zaidi.

Kwa upande wake mwanzilishi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Abulsamad Abdulrahim amesema, dira na sera vimebadilika katika kuweka uimara katika sekta ya Mafuta, gesi na nishati kwa ujumla katika uongozi wa awamu ya sita unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Abdulsamad amesema, katika maadhimisho hayo wamejadili mada kwa kuhusianisha na miradi mbalimbali inayoendelea ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga Tanzania mradi wenye fursa lukuki kwa watanzania.

Pia amesema kuwa katika mjadala huo wamebainisha miradi zaidi 30 yenye fursa kwa wasimamizi wa miradi zaidi ya 200 nchini pamoja na kujadili namna bora zaidi ya kutekeleza miradi inayoendelea nchini kwa kiwango cha juu kwa gharama nafuu, uaminifu na kupeperusha vyema kwa bendera ya nchi.
Kiongozi wa Biashara kutoka kampuni ya kimataifa ya usimamizi wa Miradi (Project Managemant International), George Asamani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya Usimamizi Miradi ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Novemba 5.




Wadau wa Usimamizi Miradi wakisikiliza mada wakati wa kusheherekea siku ya usimamizi Miradi ambayo hufanyika Novemba 5 kila mwaka.
Wadau wa Usimamizi wa Miradi wakiwa katika Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad