HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 10, 2021

ECOBANK TANZANIA YATOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

 

 

Ecobank Tanzania imeshiriki maonesho ya Wiki ya huduma za Fedha Kitaifa ili kuongeza uelewa kwa wananchi kwa lengo la kuchochea ustawi kwa Maendeleo ya Kijamii yenye Kauli mbiu ya “Boresha Maisha kupitia elimu ya fedha.”

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango yameanza toka Novemba 08 hadi Novemba 14 mwaka huu yanalenga wadau mbalimbali wakiwemo; watumishi wa umma, wanafunzi, wakufunzi, wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za fedha; na umma kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Serikali imepanga kutumia Fedha kwenye mitaji ya wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatoa huduma za kifedha kwenye Mpango wa Maendeleo ya sekta ya Fedha hapa nchini.

Amesema Elimu ijikite kwenye huduma za Fedha ili waweze kukuza kipato cha mtu mmojamoja na kuongeza mapato kwa taifa hivyo ni vyema kujipima ipasavyo ili kuongeza ufanisi kwenye huduma za kifedha hapa nchini.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Masoko na Mawasiliano Ecobank Furaha Samalu amesema Benki hiyo imeshiriki katika maonesho hayo ili kuweza kitangaza huduma wanazozitoa ili kuweza kupanua wigo kwa wananchi hasa wajasiriamali wadogowadogo.

Poa amesema Ecobank Tanzania wanatoa huduma za kifedha kama vile kufungua akaunti, huduma ya benki kwa njia ya wakala, kubadili Fedha za kigeni, bima pamoja mikopo pamoja na huduma ya Ellevate kwa ajili ya kuinua Biashara zinazowahusu wanawake hii yote ikiwa ni kuwafikia wananchi wote na kutoa huduma iliyobora.

Amewakaribisha wananchi kutembelea Banda la Ecobank Tanzania ili kuweza kupata elimu ya kifedha kutoka kwenye benki hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa.
Afisa Mauzo wa Ecobank Tanzania, Neema Mbiru(kushoto) kitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Mauzo wa Ecobank Tanzania Neema Yonah Kondowe(kulia)  akitoa ufafanuzi kuhusu akaunti za watoto kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la Ecobank Tanzania kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo yaliyozinduliwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Jamal Kassim Ali.
Maafida mauzo wa Ecobank Tanzania wakigawa vipeperushi mara baada ya kutoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Ecobank Tanzania wakati wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.
Elimu ikiendelea kutolewa kwenye Banda la Ecobank Tanzania leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa Wateja, Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, 
Furaha Samalu(kushoto) pamoja na na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Ecobank Tanzania Juma Hamisi(kulia) wakiwa kwenye Bada la Benki hiyo wakati wa maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad