HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 29, 2021

WAZIRI WA KILIMO PORF ADOLF MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA USAID BI KATE SOMVONGSIRI JIJINI DODOMA

 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi Kate Somvongsiri akimkabidhi zawadi mwenyeji wake

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi Kate Somvongsiri mara baada ya kumaliza mazungumzo katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Jijini Dodoma, tarehe 28 Octoba 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi Kate Somvongsiri mara baada ya kujadili kwa kina juu ya ushirikiano wa sekta ya kilimo katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Jijini Dodoma, tarehe 28 Octoba 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akimueleza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi Kate Somvongsiri kuhusu

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda tarehe 28 Octoba 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi Kate Somvongsiri katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo wamejadili kwa kina kuhusu vipaombele vya serikali katika wizara ya kilimo.

Pia wamejadili umuhimu wa kutatua tija na uzalishaji mdogo kwenye mazao ya wakulima ili kutafuta muarobaini wa kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini.

Kadhalika wamejadili umuhimu wa kuongeza nguvu na umuhimu katika sekta ya utafiti ili kubaini nini kinahitajika katika ardhi ya kilimo katika maeneo mbalimbali ya wakulima nchini ili wakulima waweze kutambua mazao yanayokubalika katika maeneo yao pamoja na kutambua aina na kiasi cha mbolea kinachohitajika.

Vilevile majadiliano hayo yamejikita Zaidi kuhusu umuhimu wa kuboresha huduma za ugani, ambapo Waziri Mkenda ameeleza kuwa tayari wizara yake imeanza kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuwawezesha maafisa ugani kuwa na Pikipiki ambazo zitawarahisishia kuwafikia wakulima kwa wakati.

Aidha, katika mazungumzo hayo wamejadili umuhimu wa Ugharamiaji wa kilimo (Agro Financing), pamoja na kuwekeza kwenye Kilimo Anga.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID Bi Kate Somvongsiri amemueleza mwenyeji wake Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda kuwa USAID dhamira ya kushiriki katika kikao kazi hicho ni pamoja na kukutana nae ili kujitambulisha kwake kujua vipaombele vya Wizara na kuandaa mkakati wa namna ya kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za Kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad