HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 12, 2021

Tigo na Samsung wazindua Z series

 
Mkuu wa kitengo cha maduka na bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga (kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), simu janja mpya aina ya Samsung Galaxy Z Fold3 na ZFlip3 ) mpya zilizozinduliwa nchini Tanzania kwa ushirikiano na Kampuni ya Samsung Tanzania. pembeni yake ni Meneja wa Samsung Electronics Tanzania, Suleiman Mohamed.
Dar es Salaam. Oktoba  12, 2021. Kampuni inayoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo kwa kushirikiana na Samsung Electronics wamezindua Simu janja aina ya Samsung Galaxy Z Fold3 na ZFlip3.

Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuongea matumizi ya mtandao wa 4G na kuchangia ukuaji wa teknolojia ya kidigitali nchini.
 
Mkuu wa kitengo cha maduka na bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo alisema “Ni jambo la kubwa sana kwetu kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza kuzihifadhi na kuuza simu za Samsung Galaxy Z Fold3 na ZFlip3 kwenye soko la Tanzania.Hii inaonesha imani yao kwetu juu ya chaneli kubwa za usambazaji tulizonazo na pia kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya juu,”alisema Myonga.

 “Lengo letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali katika maisha ya watu hapa nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili kuongeza idadi ya umiliki wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii,” alisema Muyonga.

Muyonga aliongeza “Tunalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku tukihakikisha wateja wetu wanafurahia huduma za kidigitali kupitia mtandao mkubwa wa 4G hapa nchini.Na ndio maana tunatoa 96 Gb za intaneti kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonununa Samsung Galaxy Z Fold3 na ZFlip3,” alisema .

Akizungumza wakati wa  uzindizu huo, Meneja wa Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung imezindua simu ya Samsung Galaxy Z Fold3 na ZFlip3 toleo jipya ulimwenguni ya simu janja zinazo jipinda ambayo itabadilisha namna ambavyo watu wanavyoishi na kuufurahia ulimwengu.

“kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya mawasiliano na namna watu wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu.Samsung inahakikisha inatoa teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana na mabadiliko hayo.Kwa kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila tukio na kuungana na uwapendao bila mipaka,” alisema Mohamed.

Samsung Galaxy ZFlip3 itauzwa 2,450,000Tshs na ZFold3 itauzwa 4,400,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad