HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 21, 2021

TANZANIA KUTUMIA MKUTANO WA TATU WA WANAWAKE URUSI KUZIDI KUWEZESHA WANAWAKE

 

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma Magwiza akishiriki katika moja ya mkutano katika Mkutano wa tatu wa Wanawake nchini Urusi uliofanyika Oktoba 13-15 jijini Saint Petersburg.

Na WAMJW Saint Petersburg Urusi
 TANZANI imeazima kuendelea kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uongozi na uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia Majukwaa ya uwezeshaji wanawake Kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma Magwiza wakati akizungumzia namna Tanzania ilivyojifunza kutokana na Mkutano huo wa wanawake nchini Urusi.

Bi. Mwajuma amesema kuwa Tanzania imejifunza kuwa Wanawake wanaweza kushiriki katika Sekta mbalimbali na kutoa mchango wao kwenye Sekta husika na kutumia fursa hizo kupata ajira na kuajiri wengine.

Ameongeza kuwa Tanzania inahimiza Wanawake kushiriki katika uchumi wa viwanda ila kutokana na Mkutano huo imeleta changamoto mpya za kuangalia maeneo ambayo wanawake wanaweza kushiriki ili kupata fursa za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni sanaa ya uigizaji, ulimbwende na michezo ambapo wanawake wanaweza kushiriki vizuri iwapo kutakuwa na mazingira mazuri yanayoweza kuwa na tija kwenye maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

"Katika Sekta hizi inabidi tuangalie ni maeneo yapi na yana changamoto gani kwa wanawake ili tuwasaidie waweze kufika Kimataifa katika Sekta hizo" alisisitiza Bi Mwajuma

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeshaanza na inaendelea kuwawezesha wanawake katika Uongozi na majukwaa ya Uwezeshaji Kiuchumi kwenye ngazi za Wilaya na Mkoa ili kuweza kuwapa fursa katika Sekta mbalimbali.

"Nimejifunza kuwa katika kila eneo ambalo mwanamke anafanya kazi inatakiwa kupaangalia na kuona ana changamoto zipi na kumuwezesha ili aweze kuinuka Kitaifa na Kimataifa" alisema Bi. Mwajuma

Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Tatu wa Wanawake nchini Urusi uliofanyika nchini humo kuanzia tarehe 13-15 Oktoba 2021 ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Dorothy Gwajima alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad