Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na waandishi wa habari.
Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, wamewataka
wananchi wa eneo hilo kuepuka utapeli wa viwanja kwenye eneo la Maisaka
Kati maarufu kama makatanini hivyo wakitaka viwanja wafike kwenye ofisi
za halmashauri ya Mji wa Babati.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake wakati akisoma taarifa ya kipindi cha
miezi mitatu ya tangu mwezi Julai hadi Septemba amesema wananchi
wachukue tahadhari ili kuwaepuka matapeli hao.
Makungu
amesema wamekuwa wakipokea malalamiko kadhaa ya baadhi ya kampuni
zinazojiita za udalali zikilalamikiwa kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kupitia mradi wa viwanja vilivyopimwa na halmashauriya mji
vikiwemo vitalu RR na TT.
Amesema
kampuni nyingi zimekuwa zikiwalaghai wananchi kuwa zimekasimiwa mamlaka
ya kuuza viwanja hivyo na kwa njia hiyo kujipatia fedha nyingi kwa
kuuza viwanja kuliko bei halali.
“Imebainika
kuwa baada ya kulipa fedha kwa madalali hao, wananchi waliotapeliwa
fedha zao huelekezwa kwenda ofisi za halmashauri ya mji kwa ajili ya
kukamillisha taratibu za kupatiwa hati, lakini wanapofika kwenye ofisi
hizo hugundua kuwa wametapeliwa,” amesema Makungu.
Hata
hivyo, amesema kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita elimu kwa umma
imetolewa kwa jumla ya semina 40 zilizoendeshwa kwa makundi tofauti ili
kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.
Amesema
jumla ya mikutano 24 ilifanyika ikiwa na madhumuni ya kuelezea athari
za rushwa na jinsi ya kupambana nayo ambapo jumla ya klabu 35 za wapinga
rushwa katika shule za sekondari zilitembelewa kwa lengo la
kuziimarisha na kupatiwa mafunzo na vipindi tisa vya redio vyenye
maudhui ya mapambano dhidi ya rushwa na ofisi ilishiriki na kufanya
onyesho moja.
“Ndugu
wanahabari, katika kipindi cha miezi mitatu cha Oktoba hadi Desemba
mwaka huu tutaendelea na zoezi la kudumu la ufuatiliaji wa utekelezaji
wa miradiya maendeleo ili kuhakikisha kuwa inaakisi thamani ya fedha
iliyopangwa,” amesema Makungu.
Ametoa
rai kwa wana Manyara kuendelea kutoa taarifa za rushwa kwa kupitia
namba zao za dharura 113 au kwa kufika ofisi zao zilizo karibu nao
kuunga mkono kauli mbiu isemayo “Kupambana na rushwa ni jukumu langu-
Kazi Iendelee.”
No comments:
Post a Comment