Na Khadija Kalili, Kibaha
JESHI
la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wawili jamii ya wafugaji
kwa tuhuma za kumpigia na kumjeruhi Mwenyekiti wa Chama Cha
Umwagiliaji Mpunga (CHAURU), Ruvu Mkoani Pwani aliyetajwa kwa jina la
Sadaka Chacha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani ACP Nyigesa Wankyo kuwa Oktoba 25 saa tisa alasiri katika
mashamba yanayomilikiwa na Chama Cha Umwagiliaji Ruvu (CHAURU)
watuhumiwa hao wakiwa na wenzao watatu jumla walikua watano
walilazimisha kuingiza mifugo Yao kwenye mabwawa ya kilimo cha
Umwagiliaji Ili mifugo yao inywe maji.
RPC
Wankyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Petro Ngilangu (25)na Robert
Kambai (28) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji Cha Kidogozelo Kata ya
Vigwaza.
Wafugaji hao walimshambulia Mwenyekit huyo wa CHAURU Chacha kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani.
Tukio
la kupigwa lilitokana baada ya Mwenyekiti huyo akijaribu kuzuia mifugo
kuingia ndani ya mashamba hayo, ambapo Sadala akiambatana na Daniel
Mwita Ofisa pamoja na askari Mgambo walielekea eneo hilo.
Walipofika
mashambani Askari Mgambo walipoona wamezidiwa walitimua mbio na
kuwaacha wenzao ndipo wakawavamia Chacha na Mwita wakawashambulia kwa
kutumia fimbo na vitu vyenye ncha kali.
No comments:
Post a Comment