HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 4, 2021

Phoenix Assurance yazindua huduma mpya ya Bima ya Utulivu

 



 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Phoenix, Ashraf Musbally ( wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya ‘Utulivu’ ambayo watapewa wateja wao wenye bima kubwa. Wa pili kushoto ni Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) Hillard Maskini na wapili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha Trafiki Makao Mkuu Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mossi Ndozero. Kulia ni ni Godfrey Badeleya ambaye ni mkuu wa kitengo cha fedha na Utawala na mifumo wa kampuni ya Bima ya Phoenix. Huduma ya Utulivu ambayo kazi yake kubwa ni kuwasaidia wateja wanapopata matatizo mbalimbali wakiwa kwenye vyombo vya moto (magari)


Meneja Mkuu wa kampuni ya Bima ya Phoenix (Phoenix Assurance) Godfrey Badeleya (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Utulivu ya kampuni hiyo. Huduma ya Utulivu ambayo kazi yake kubwa ni kuwasaidia wateja wanapopata matatizo mbalimbali wakiwa kwenye vyombo vya moto (magari).


Maofisa wa kampuni ya Bima ya Phoenix wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) na Jeshi la Polisi (Trafiki) mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Utulivu ambayo kazi yake kubwa ni kuwasaidia wateja wanapopata matatizo mbalimbali wakiwa kwenye vyombo vya moto (magari).



Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya Bima ya Phoenix Issurance imezindua huduma ya Utulivu kwa lengo la kuwasaidia wateja wao wanapopata matatizo mbalimbali wakiwa kwenye vyombo vyao vya moto (magari).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Phoenix, Ashraf Musbally amesema kuwa huduma hiyo ni ya bure kwa wateja wao wa bima kubwa ya magari (comprehensive).

Bw. Musbally alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya moto wanakutana na changamoto nyingi ikiwa kama kuharibikiwa na magari, kupata pancha, kuishiwa mafuta, kusahau funguo na nyinginezo ambazo wao watazifanya bila ya gharama yoyote.

“Lengo la kutoa huduma hii ni kuwapa utulivu wateja wetu wanapokabiliana na matatizo mbalimbali wakiwa barabarani na hata nyumbani kwao.

Unaweza kukuta gari lako limepataa kuwaka, unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwetu na mafundi watakuja kufanyia matengenezo hapo hapo nyumbani kwako,” alisema Musbally.

Alisema kuwa mipango yao ni kutoa huduma hii mikoani kwa wateja wao hata wa mikoani katika siku za hizi karibuni.

“Hii ni huduma ya ziada, haina malipo yoyote ambapo mteja wetu wa bima kubwa atafaidika nazo, nawaomba wateja wetu wa bima nyingine kufanya.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Phoenix Assurance Robert Kalegeya amesema kuwa wameamua kutoa huduma hiyo kama kuwafariji wateja wao ili waendelee kufanya nao kazi.

Bw Kalegeya alisema kuwa biashara ya bima ina ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa makampuni mengi hapa nchini.

Alisema kuwa kutokana na ushindani huo, kampuni yao imeamua kuwa na ubunifu wa kutoa huduma mbalimbali ili kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Meneja wa Leseni na Usimamizi wa mwenendo wa soko wa mMamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) Hillard Maskini aliipongeza kampuni hiyo ya Bima kwa kuanzisha huduma hiyo bora kabisa.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha Trafiki Makao Mkuum Mrakibu wa Jeshi la Polisi Mossi Ndozero alisema kuwa huduma hiyo ina lengo la kudumisha usalama wa wateja ambao jeshi la Polisi linasisitiza


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad